Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras ametangaza kupunguza kodi na kuongeza malipo kwa wastaafu.
Tsipras amesisitiza kwamba Serikali ya Ugiriki inawekeza katika sera za kijamii na kiuchumi na kuwa itayatimiza majukumu yake na kulipa mikopo iliyopokea.
Kutokana na mzozo wa kiuchumi uliokuwa unaikabili Ugiriki mwaka 2012 na uliopelekea nchi hiyo kukopa sana, nchi hiyo iliagizwa kuchukua hatua za dharura za kuweka akiba ya kifedha na miongoni mwa hatua hizo ilikuwa ni kupunguzwa kwa malipo uzeeni.