29.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

SERIKALI YA NEW ZEALAND KUFANYA MBADILIKO YA SHERIA YA BUNDUKI

CHRISTCHURCH, New Zealand

Serikali ya New Zealand ina mpango wa kufanya mabadiliko ya sheria ya bunduki wiki ijayo ili kukabiliana na mashambulizi ya misikiti miwili huko Christchurch wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Jacinda Ardern, sheria hizo zinaweza kujumuisha kuzuia silaha za kisasa za kijeshi ambazo zilitumiwa katika mashambulizi, ambayo yameua watu 50 na wengine 40 kujeruhiwa, na ambazo zimekuwa zikitumika sana hivi karibuni nchini Marekani.

Kwa mujibu wa ripoti zilizopo ni kwamba idadi ya vifo vinavyotokana na mashumbulizi kama hayo zinazidi mwaka hadi mwaka ukitolewa mfano wa karibu wa mwaka 2017 nchini New Zealand ambapo watu 35 waliuawa.

“Mashambulizi ya kigaidi haya ni mabaya sana katika Pwani yetu na yameonyesha idhaifu mkubwa katika sheria za bunduki New Zealand. Somo la wazi kwa historia duniani kote ni kwamba, ili kufanya jamii yetu salama, wakati wa kutenda ni sasa, “Ardern alisema

Aliongeza kuwa Baraza la Mawaziri litakaa na kulifanyia kazi suala hilo na atatoa mrejesho kabla ya kukaa kikao kingine siku ya Jumatatu ya wiki ijayo.

 â€śNdani ya siku 10 baada ya tukio hili la kigaidi, tutakuwa tumeshatangaza mabadiliko katika sheria hihyo ambayo ninaamini yataifanya jamii yetu kuwa salama, alisema Arden.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles