24.6 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali ya Congo yaridhia kuchukua shehena ya mafuta bandari ya Tanga

                                  Susan Uhinga, Tanga



Ujumbe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ukiongozwa na Waziri wa Mafuta wa nchi hiyo Ngoi Mukena wamefika Mkoani Tanga, kujionea Uboreshwaji wa miundombinu ya Bandari  na wa  ya kampuni ya GBP ambao ni waingizaji wa mafuta nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari waziri huyo amesema amefurahishwa na miundombinu ya kisasa katika kampuni ya GBP pamoja na uboreshwaji wa Bandari ya Tanga.

” Nimefurahishwa na kwa hakika sasa tunaona umuhimu wa kutumia bandari ya Tanga kuchukua mafuta na kuyaleta nchini kwetu niseme nimeridhishwa” amesema.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Bandari Mkoani Tanga Donald Ngaile amesema kwa sasa mchakato wa upanuzi wa bandari ya Tanga unaendelea na tayari upimaji wa miamba iliyoko chini ya bahari umeshafanyika.

“Kwa sasa Bandari yetu ina uwezo wa kuhudumia hata nchi za jirani hivyo tunawakaribisha wenzetu wa Congo watumie bandari yetu kwani tuna uwezo wa kuwahudumia vizuri na kwa wakati” amesema.

Naye Muwekezaji wa Kampuni ya uingizaji wa mafuta Nchini (GBP), Sudi Badar  ameishukuru serikali ya Rais Magufuli kwa kusimamia mifumo mizuri ya uwekezaji ambayo itawezesha kampuni kuhudumia na nchi jirani na Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles