30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali, wapinzani wavutana kuzikwa upya Savimbi

LUANDA, ANGOLA

MZOZO umeibuka baina ya Serikali  na upinzani nchini hapa  juu ya mipango ya kuzika upya mwili wa aliyekuwa kiongozi wa vuguvugu la waasi wa Unita, ambaye kifo chake kilitokea miaka 17 iliyopita na kumaliza vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu kwa karibu miongo mitatu.

Awali Serikali ilikuwa inataka kuukabidhi mwili wa Savimbi kwa wawakilishi wa Unita, ambacho sasa ni chama cha upinzani, ili waweze kuuzika nyumbani kwao Juni mosi, lakini  makabidhiano  hayakufanyika na kila upande sasa unamlaumu mwingine.

Helena Savimbi, mmoja wa watoto wa kike wa kiongozi huyo wa waasi, aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa – AFP kwamba Serikali haikuheshimu mkataba na ndiyo maana ukaibuka  mkanganyiko mkubwa.

Kwa upande wake, Serikali nayo imeishutumu Unita kwa kushindwa kuuchukua mwili Jumanne, kama walivyokubaliana.

 Waasi wa Unita wakiungwa mkono na Marekani na Afrika Kusini, walipambana na wapiganaji wa Angola wa MPLA kwa miaka 27 katika mzozo wa vita baridi uliodumu kwa muda mrefu.

Savimbi aliuawa katika mapigano na Serikali mwaka 2002, na kuzikwa katika Jimbo la Moxico lililopo magharibi mwa nchi hii.

Kifo chake kiliwezesha kufikiwa kwa mkataba wa amani na hatimae kujumuishwa kwa waasi wa Unita katika mchakato wa kisiasa.

Kikiwa ndio chama kikuu cha upinzani, Unita kimekuwa kikifanya kampeni ya kutaka mwili wa Savimbi uzikwe kwa heshima.

Mwili wake uliofukuliwa ulitakiwa kukabidhiwa na Serikali kwa Unita katika mji wa Luena, ambao ni mji mkuu wa jimbo hilo la la Moxico, Jumanne wiki hii.

Hata hivyo kwa mujibu wa msemaji wa Unita, Alcides Sakala Simoes, Serikali ilibadili katika dakika za mwisho ikisema makabidhiano hayatafanyika.

“Hatujui ni wapi mwili ulipo … Wanataka kuikatisha tamaa Unita,” msemaji huyo aliiambia  AFP. 

“Hii haitasaidia mchakato wa ujenzi wa taifa,” aliongeza.

Hata hivyo, waziri wa masuala ya kitaifa, Pedro Sebastiao amepuuzia mbali kauli hizo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Taifa, mwili umekwishapelekwa Luena kama ilivyopangwa, lakini Unita haikuwepo kukabidhiwa mwili na umeachwa katika kambi ya jeshi ukisubiri kuchukuliwa na chama hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles