26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Serikali, wananchi waombwa kumsaidia kijana Elia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Shule ya Msingi Lusasaro iliyoko Tabata Kisukuru jijini Dar es Salaam imewaomba Watanzania na Serikali kwa jumla kumsaidia mtoto yatima, Elia Hubert (14) aliyemaliza shuleni hapo.

Mwalimu wa Taaluma wa Shule hiyo, Maganiko Simon anasema kwamba shule yake imemsomesha mtoto huyo bure elimu ya msingi na kuweza kufaulu vizuri na kuchaguliwa kujiunga shule ya serikali ya kutwa ya Bagozalakini changamoto ni uwezo duni wa familia yake ambayo haiwezi kumudu gharama za elimu za kijana huyo.

“Naiomba serikali imsaidie ikiwamo kumpangia shule ya bweni na pia nawaomba Watanzania wamchengie kijana fedha za kumuwezesha kumudu gharama mbalimbali za elimu kupitia namba 0756 729 019 majina ya Mpokeaji ni Joyce Ngalula,” amesema Simon.

Naye mama Mlezi wa Kijana huyo, Saada Hussein anawaomba Watanzania wamchangie kijana huyo ili aweze kumudu gharama za elimu huku akiiomba serikali impangie kijana huyo shule ya bweni kwani familia yake haina uwezo hata wa kumpa nauli na malazi kijana huyo ikiwamo nauli za kila siku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles