32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI: WAKULIMA WADOGO WAPEWE MIKOPO

Na MWANDISHI WETU-BUKOBA



WITO umetolewa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kutoa mikopo kwa walengwa wa Benki hiyo ambao ni wakulima, wafugaji na wavuvi wadogo nchi nzima, ili kuweza kuwakwamua katika changamoto zinazorudisha nyuma juhudi zao za kujiongezea kipato kwa kukosa mitaji ya uhakika katika kuongeza tija ya kilimo nchini.


Hayo yalisemwa juzi mjini hapa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Tate ole Nasha, wakati akifungua rasmi maadhimisho ya Kampeni ya Wiki ya Maziwa inayofanyika kitaifa mjini Bukoba, mkoani Kagera.


Alisema dhima ya kuanzishwa kwa TADB ni kutoa suluhisho la ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha na mikopo kwa wakulima wadogo nchini, ili kuchagiza maendeleo ya kilimo nchini, hivyo Benki ina wajibu wa kuwafikia wakulima wote wadogo wenye uhitaji wa mikopo.
“Nawaomba mjielekeze kutoa mikopo yenu ya gharama nafuu kwa wakulima wadogo ambao hawawezi kupata mikopo kwenye benki za biashara ili kutekeleza lengo la Serikali la kuwainua wakulima kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara, ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini,” aliseka ole Nasha.


Aliongeza kuwa, anafahamu kuwa Serikali ikishirikiana na TADB ilifanya mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na kupelekea Bodi ya Benki ya Maendeleo Afrika kutoa kibali cha kuipatia TADB fedha za kukopesha kwenye sekta ya kilimo, na kuitaka Benki hiyo kutumia fedha hizo kwa kuwapatia wakulima wadogo ambao ni wahitaji zaidi wa miko hiyo.


TADB ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha za mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini, ambao ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa, riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles