21.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Serikali mbioni kununua ndege ya mizigo

Anna Potinus

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema serikali imeshaanza mazungumzo ya namna ya kupata ndege ya mizigo kwaajili ya kubeba mazao ya mbogamboja kuyepaleka nje ili kuwasaidia wakula.

Ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano Novemba 13, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini aliyetaka kujua mkakati wa serikali katika kutafuta ufumbuzi wa masoko ya mazao ya mbogamboga.

“Jimboni Rombo tunalima sana maparachchi na yananunuliwa na wafanyabiashara walanguzi kutoka Kenya, kilimo hiki cha hot culture Kaskazini huko wakulima wanapata hasara kubwa, sasa katika mkakati wa kutafuta masoko ni kwanini tusiangalie uwezekano kama nchi kununua ndege ya mizigo itakayosaidia wakulima wetu nje ya nchi kwasababu mazao haya ya mbogamboga yanakwenda Nairobi na kusafirishwa na ndege za Kenya,” amehoji.

Akijibu hoja hiyo Waziri Kamwelwe amesema serikali imeshafanya mazungumzo juu ya suala hilo na kwamba wana mpango wa kuanza kukodisha ndege kwaajili ya kusafirisha mazao hayo na minofu ya samaki kutoka Mwanza.

“Tayari tuna miezi mitatu tulishaanza kujadiliana kuhusiana na jinsi ya kupata ndege ya mizigo kwaajili ya kubeba mazao ya hot culture Uwanja wa Ndege wa Songwe pamoja na minofu ya samaki kutoka Mwanza kwahiyo tutaanza na kukodi ndege kwasababu tuna changamoto ya mzigo wa kutoka Europe kuja huku lakini kutoka hapa kwenda kule mzigo upo,” amesema Kamwelwe.

Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema serikali imekuwa ikihamasisha wakulima na wadau wengine kuongeza uzalishaji wa zao la parachichi hususan aina ya hass, kutekeleza mkakati wa kuainisha maeneo yote yanayofaa kwa kilimo hicho nchini pamoja na kuongeza uzalishaji wa miche ya maparachichi aina ya hass na kuilinda ili isiharibiwe na aina nyingine za mapachichi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,717FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles