28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI KUWEKEZA HALI YA HEWA


Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali itaendelea kuiwezesha Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), kuwa na vifaa na mitambo ya kisasa ya hali ya hewa ili kurahisisha huduma bora za utabiri kutolewa kwa wakati.

Profesa Mbarawa amesema hayo mjini Dodoma leo Ijumaa Machi 23 na kusisitiza kuwa kwa sasa TMA imeongeza imani kwa wananchi kwani imekuwa ikitoa utabiri wa kuaminika kwa  sababu ya kuwa  vifaa vingi na vya kisasa vya utoaji taarifa.

“Serikali itaendelea kuwezesha TMA na kuhakikisha inatoa utabiri sahihi na wa uhakika kwani kuwepo kwa utabiri sahihi kuwawezesha vyombo husika kuchukua hatua mapema kabla ya madhara makubwa kutokea,” amesema.

Aidha, amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kuacha kulima kwenye vyanzo vya maji na kuepuka kuchafua maeneo ya bahari ili kuepusha athari zinazoepukika zikiwemo uharibifu wa miundombinu ya  uchukuzi.

“Nawaomba wananchi wote watunze mazingira kwani kumekuwa na uharibifu mkubwa wa miundombinu kutokana na shughuli zinazofanywa na binadamu katika maeneo mbalimbali yasiyotakiwa kulimwa au kujengwa, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi amesema serikali inajitahidi kuwekeza kwenye miundombinu ya hali ya hewa kwa kutoa fedha kununua vifaa mbalimbali ambavyo vimewezesha mamlaka hiyo kutoa utabiri sahihi kwa zaidi ya asilimia 70.

“Kwa sasa utabiri wa usafiri wa anga ni wa uhakika kwa asilimia 90 na hutolewa kila baada ya nusu saa na marubani hupata taarifa hizo kwa wakati kabla ya kuanza safari zao, amesema Dk. Kijazi.

 


 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles