27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 16, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI KUWATAMBUA WANANCHI HIFADHI YA SAADANI

Na Suzan Uhinga, Tanga

Serikali iko kwenye mchakato wa kutengeneza vitambulisho maalumu vya kuwatambua wananchi wanaoishi pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Saadani  (Sanapa) kama njia rahisi ya kuwatambua.

Waziri wa Maliasili na Utalii Nchini Dk. Hamisi Kigwangwala amesema hayo wakati mkoani Tanga, ambapo amesema hatua hiyo inatokana na changamoto ya ujangili katika maeneo ya hifadhi.

“Serikali imeamua kuwatengenezea wananchi hao vitambulisho maalumu vitakavyowatambulisha kuwa ni majirani wa eneo la hifadhi ili wasibughudhiwe .

Pamoja na mambo mengine, hatua hiyo imekuja mara baada ya malalamiko ya Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete kutoa malalamiko ya wanachi kwamba wananyanyasika kwa kudaiwa fedha mara wanapoingia hifadhini hata wanapokuwa katika shughuli zao za kawaida za kila siku.

“Mheshimiwa Waziri wananchi wamekuwa wakinilalamikia kwamba wanatozwa fedha na askari wa wanaolinda hifadhi wakati wakivuka kupita hifadhini kwa shughuli zao za kila siku hivyo naomba tulitafutie ufumbuzi ili wananchi waweze kuondokana na kero hii,” amesema Mbunge huyo wa Chalinze.

Amesema wananchi wanaoishi eneo hilo wanatambua umuhimu wa hifadhi hiyo na wanasaidia utunzaji wa mazingira ya hifadhi hivyo serikali ione namna ya kuwaondolea kero hizo.

Kwa upande wake muwakilishi wa Mkurugenzi wa uhifadhi Martin Laiboko amesema wamelipokea agizo hilo kutoka kwa waziri na kwamba watalifanyia kazi lengo likiwa kujenga ujirani mwema na hifadhi endelevu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles