31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuunda baraza la waandishi kujisimamia wenyewe

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abasi, amesema serikali iko kwenye hatua za mwisho kuanzisha Baraza Kuu la Habari ambalo litakuwa chombo kikuu na cha juu cha kuwaunganisha waaandishi wa habari pamoja.

Akizungumza wakati akiwasilisha mada kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini (Tudarco), jijini Dar es Salaam, kutoka vitivo mbalimbali kikiwamo cha Mawasiliano kwa Umma, kuhusu Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2016, Dk. Abasi amesema baraza hilo pamoja na mambo mengine watakuwa na kazi ya kuonyana.

“Tunavyo vyombo vingi vingine vya aina hii vinafanya kazi tunavishukuru, lakini hili ndiyo litatambulika kwani wanahabari wana vyama vingi lakini hawana chama au chombo kimoja imara cha kutetea maslahi yao.

“Pamoja na kuwa chombo cha kuwanunganisha wanahabari pamoja, lakini baraza litafanya kazi maalumu kubwa ambayo itawafanya wanahabari kuonyana wenyewe kwa wenyewe kwani kuna mambo yakitokea kwa sasa wanakuja serikalini kwa sasa tunataka wanahabari wajisimamie wenyewe,” amesema.

Amesema awali kabla ya sheria hii, mambo yote hayo kabla ya sheria hii yalikuwa yanakwenda serikalini lakini kwa sasa mambo yanayoshusu wanahabari yanarudi kwao wenyewe kupitia chombo chao na serikali ibaki na mambo ya machache yanayohusu uslama wa nchi.

Dk. Abasi amesema taaluma ya habari ni taaluma yenye muktadha mpana ambapo ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wanahabari kuenzi taaluma yao.

“Yako mambo ambayo wanataaluma tunapaswa kuyatafakari kuna vyombo vingi kwa sasa, Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na tumesajili mikataba mingi ya kimataifa kama kuna matukio machache kwa wanahabari kupata matatizo serikali imekuwa ikiyafanyia kazi,” amesema.

Aidha, akizungumzia lengo la kuwasilisha mada hiyo kwa wanachuo hao, Dk. Abasi amesema ni kuhakikisha wanahabari wasomi hata kama wanasoma darasani lakini ni muhimu wakasikia kutoka kwa watekelezaji wenyewe.

“Tumejadiliana kifungu kwa kifungu katika mambo ambayo walipaswa kuyajua, muswada umeshakuwa sheria kamili tunakwenda kuunda Bodi ya Ithibati kwa mfano kusajili wanahabari kuwa wanataaluma kamili kama ilivyo kwa wanasheria na wakandarasi.

“Na hii ni historia kwa nchi yetu tuliozea kuona wanahabari taaluma inadharauliwa kama mwajiri anaweza kukuita na kukufukuza wakati wowote lakini hii inampa heshima kwa jamii na mwajiri,” amesema Dk. Abasi.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara Mawasiliano kwa Umma cha chuo hicho, Dk. Darius Mukiza, amemshukuru Dk. Abasi kwa mada hiyo na kumtaka kutosita kurejea tena kwa mada mbalimbali zinazohusu taaluma ya habari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles