27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kutumia Ndege kudhibiti nzige Longido

Na Mwandishi Wetu, Longido

Serikali imewatoa hofu wananchi wa maeneo ya Longido na kuwataka wasiwe na hofu kufuatia nzige walioovamia wilayani humo wakitokea nchi jirani ya Kenya.

Hayo yamebainishwa na jana Februari 21, na Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda, baada ya kutembelea eneo la Longido ambalo limevamiwa na nzige  na kuwa kuanzia leo ndege maalum itafanya kazi kupulizia viuatilifu kuua nzige hao.

Prof. Mkenda amesema wananchi wasiwe na hofu nzige wote watadhibitiwa kupitia wataalam wa Wizara ya Kilimo waliopo kwenye maeneo yote yenye dalili za uwepo wa wadudu hao.

“Kuanzia kesho (22.02.2021)  ndege maalum itaanza kazi kupulizia sumu kuua nzige waliovamia maeneo ya Longido na Simanjiro,” amesema Prof. Mkenda.

Waziri Mkenda amesema tayari wataalam wa Taasisi ya Utafiti wa viuatilifu vya  kudhibiti visumbufu (TPRI) wapo wilayani Longido na Simanjiro wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wake Dk. Efrem Njau. .
Aidha ametoa wito kwa wananchi kutookota wala kula nzige watakaokuwa wameuawawa na viuatilifu(sumu) kwenye maeneo yote ambapo ndege itapita kuua nzige.

Pili, ameagiza wataalam na Watendaji wa vijiji na Kata kutoa taarifa Kwa wananchi juu ya uwepo wa kazi ya kuua nzige hivyo wasiwe na hofu.

“Wananchi wakiona nzige wameanguka chini wamekufa wasiwachukue au kula kwa kuwa wengi watakuwa wamekufa kwa sumu,” amesisitiza Prof. Mkenda.

Waziri huyo wa kilimo amesisitiza kuwa serikali itahakikisha mazo ya wakulima na malisho ya Mifugo hayaribiwi na nzige ndio maana ametembelea eneo hili la Longido ambapo amebainisha mafanikio ya kuwadhibiti tangu walipoingia nchini mwezi Januari mwaka huu kwenye baadhi ya maeneo.

Prof. Mkenda amesema nzige wa jangwani wana athari kubwa katika uzalishaji wa mazao ya chakula  na malisho ya mifugo na kundi moja la nzige lina uwezo wa kuruka  bila kutua kwa umbali wa  kilometa 150 Kwa siku.

Aidha, nzige wana uwezo wa kula Sawa na uzito wake  kwa siku ambapo kundi moja la nzige linaweza kuwa na wastani wa nzige milioni 40 kwenye eneo la kilometa  moja za mraba alisema Waziri Mkenda .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Jumaa Mhina, ametoa agizo shule zote za msingi na sekondari kwenye maeneo ambapo ndege itapuliza viuatilifu kusitisha masomo Kwa muda wa siku 4 kuanzia kesho ili kudhidhibi watoto wasije wakapata madhara endapo watashika au kuchezea nzige watakaokufa.

Naye Mbunge wa Longido, Dk. Steven Lemomo Kiruswa, ameiomba serikali iharakishe kupulizia viuatilifu ili nzige wasije leta madhara kwa mifugo na wakulima kwenye maeneo ya Longido.

“Leo(jana) ni siku ya tatu nzige wameingia Longido, tunaomba jitihada za wataalam wa TPRI kuwadhibiti ili wasilete madhara kwetu sisi wafugaji tunaotegemea nyasi kwa malisho,” amesema Kiruswa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles