25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kutumia bil. 30/- viuatilifu vya pamba

NA SAM BAHARI -SHINYANGA

SERIKALI imepanga kutumia Sh bilioni 30 kubadili mfumo wa uagizaji wa viuatilifu katika msimu wa mwaka 2019/20 katika mikoa 17 inayolima zao la pamba nchini.   

Pia Serikali ina mpango wa kufungua vituo viwili vitakavyotumika kuzalisha mbegu za pamba vipara kwa lengo la kuboresha na kuongeza uzalishaji wenye tija katika zao hilo. 

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa mjini hapa akiwa katika ziara za kikazi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kutembelea miradi ya maendeleo na kubaini changamoto zilizopo mkoani hapa.

Bashungwa alizitaja wilaya ambako vituo hivyo vitaanzishwa ni Bariadi katika Mkoa wa Simiyu na Igunga mkoani Tabora.

Vituo hivyo vinatarajiwa kutayarisha na kuandaa mbegu za pamba vipara zitakazosambazwa katika wilaya 56 zinazolima zao hilo nchini.

Bashungwa alisema Serikali imekusudia kuvunja mkataba na nchi ya China wa kuleta viuatilifu nchini kwa asilimia 95 vinavyotumika kuulia wadudu waharibifu wa zao la pamba, na badala yake itanunua yenyewe dawa hizo na kuzileta nchini lengo ni kutafuta ubora na bei nafuu kwa wakulima.

“Serikali imekusudia kuvunja mkataba na China kutununulia viuatilifu na kutuletea hapa nchini na badala yake Serikali ya Tanzania itazinunua na kuzileta kwa wakulima lengo ni kupata dawa bora na bei nafuu,” alisema Bashungwa.

Alisema katika kipindi hiki Serikali ina mkakati na juhudi za makusudi zinazoendelea kufanyika kuanzishwa viwanda vya kuchambua pamba, kuchakata nyuzi na kuanza kutengeneza nguo, sambamba na kutengeza na kuboresha mazingira ya uwekezaji.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles