29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali kutoa taarifa hali ya chakula bungeni

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama.

Na MAREGESI PAUL, DODOMA

SERIKALI imeahidi kutoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa chakula nchini kabla Bunge halijaahirishwa Septemba 16 mwaka huu.

Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama, alipokuwa akijibu mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Kessy Mohamed (CCM).

Katika mwongozo wake, Kessy alirejea swali lililoulizwa wakati wa kipindi cha maswali na majibu na Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuokoa chakula cha wakulima kinachoharibika baada ya wakulima hao kuzuiwa kuuza chakula nje ya nchi.

Katika swali hilo, Msukuma alisema Kanda ya Ziwa wamekuwa wakilima pamba kwa miaka mingi lakini hivi sasa zao hilo halilimwi na badala yake wakulima wanalima mpunga ambao unaharibika baada ya Serikali kuzuia uuzwaji wa chakula nje ya nchi.

Kutokana na swali hilo, Kessy alipoomba mwongozo wa Spika akiishutumu Serikali kwa kile alichosema inawaumiza wakulima kwa kuwa mazao yao yanaharibika kwa ukosefu wa soko ambalo linapatikana nje ya nchi.

Mwongozo huo uliungwa mkono na MbungeĀ  wa Kwela, Ignas Malocha (CCM), ambaye alisisitiza umuhimu wa kauli ya Serikali juu ya upatikanaji wa chakula nchini.

Akijibu miongozo hiyo baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kuitaka Serikali itoe kauli, Mhagama alisema Serikali itafanya hivyo wakati wowote kutokana na umuhimu wa suala hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles