23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI KUTEKELEZA MPANGO WA KUHIFADHI WAKIMBIZI

Na LEONARD MANG’OHA

-DAR ES SALAAM

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, amewahakikishia wadau wanaoshughulikia masuala ya wakimbizi iko tayari kushirikiana nao kutekeleza Mpango wa kushughulikia wakimbizi unaolenga kuboresha huduma za kijamii na maendeleo (CRRF) katika maeneo yanayopokea wakimbizi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, ukihusisha wadau mbalimbali wa masuala ya wakimbizi, Mhandisi Masauni alisema mpango huo unatokana na makubaliano yaliyofikiwa New York, Marekani mwaka jana.

Alisema CRRF utasaidia si tu kuleta maendeleo kwa wakimbizi, bali pia kwa wananchi wa maeneo hayo katika sekta za afya elimu, afya, maji na shughuli nyingine za maendeleo.

Alisema lengo la mpango huo ni kuhakikisha nchi wahisani zinashiriki kuzipunguzia mzigo mkubwa nchi zinazopokea wakimbizi, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha zinanunua chakula cha wakimbizi hapa nchini ili kusaidia wananchi kupata masoko ya mazao yao.

Alisema tangu kufikiwa kwa makubaliano hayo, mwaka uliopita Tanzania imeendelea kuwahifadhi watu wanaotafuta makazi 75,000 na kufanya jumla ya wakimbizi na watafuta hifadhi 335,000 hadi sasa.

“Hatuwezi kuacha kupokea wakimbizi, lakini tutapokea walio salama, waliokuwa askari huko tutawaweka katika magereza hadi tuhakikishe wamebadilika tabia, haya yaliyoelezwa kwenye mpango huu mengi tumekuwa tukiyatekeleza hapo kabla, hivyo naamini hayatakuwa magumu kwetu,” alisema Mhandisi Masauni.

Mkurugenzi Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke, alisema pamoja na mambo mengine, wanatekeleza mpango wa kuhamishia wakimbizi katika mataifa wahisani, ambapo hadi sasa wakimbizi 7,000 wamepelekwa nchini Marekani, huku wengine zaidi ya 50,000 wakitarajiwa kusafirishwa baadaye.

“Lakini juhudi zaidi zinachukuliwa kuhakikisha matatizo katika nchi zao yanatatuliwa na nimshukuru Rais Mstaafu Mkapa kwa juhudi zake za kutafuta amani ya kudumu Burundi, tunataka amani itakaporejea waweze kurudi kwao,” alisema Mseke.

Aliongeza kuwa, katika makubaliano ya New York walikubaliana kutoa Sh 10,000 kwa wakimbizi 10,000, ambapo kiasi hicho kinategemewa kuongezeka hadi kufikia watu 50,000, zaidi ya dola milioni nne zitaingia katika mzunguko wa fedha na kusaidia kukuza uchumi wa nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles