23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kutatua changamoto madini ya chuma

Na Elizabeth Kilindi,Njombe.

SERIKALI imesema inatatua changamoto zinazokwamisha kuanza kwa mradi wa kimkakati wa uchimbaji na uchakataji wa madini ya chuma na makaa ya mawe yanayopatikana wilayani Ludewa mkoani Njombe.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo  alipofanya ziara mkoani hapa kwa ajili ya kukagua miradi ya uchimbaji wa madini pamoja na uwekezaji kwenye sekta hiyo.

‘’Wizara ya Madini, ndiyo itatoa leseni kwa ajili ya shughuli za uchimbaji hapa nchini…lakini pia kukamilika kwa miradi jumuishi ya makaa ya mawe ya mchuchuma pamoja na chuma cha liganga kutazalisha ajira zaidi ya 10,000,’’alisema Nyongo.

Alitaja  changamoto hizo ni  pamoja na mikataba baina ya serikali na wabia pamoja na kukamilisha utolewaji wa fidia kwa wananchi wanaotakiwa kupisha eneo la mradi.

’Fidia isihusishwe na huu mradi kwani tayari fidia katika eneo hili italipwa na serikali ili wananchi waweze kupisha eneo hili..hatua iliyofikia huko ngazi za juu utakamilika hivi karibuni fidia zitalipwa’’alisema

Alikagua  miradi jumuishi ya makaa ya mawe Mchuchuma na Liganga, mradi wa madini ya chuma inayotarajiwa kutekelezwa na serikali kwa maendeleo ya taifa wilayani Ludewa,  ambapo mipango yake tayari imeshaanza katika hatua za  awali ikiwemo utolewaji wa leseni kwa wawekezaji.

Alisema miradi hiyo, inachelewa kuanza kwa sababu ya mikataba inayohusisha serikali ikiwakilishwa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) pamoja na mwekezaji kutoka nchini China.

‘’Huu mradi ni wa siku nyingi na wenye tija kwa taifa letu na ni wa kimkakati na tumeutolea macho ili uanze changamoto ipo katika mikataba’’alisema

Naye Kaimu Mkurugenzi NDC, Pascal Malesa wamemueleza naibu waziri  ambapo alisema kuna sehemu zimeshafanyiwa kazi ambapo kuna maeneo wanayosubiri kuanza utekelezaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles