24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI KUTAIFISHA MASHAMBA YA MIRUNGI SAME

Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amesema serikali imeanza kuainisha mashamba ya watu wanaojihusisha na kilimo cha dawa kulevya aina ya mirungi katika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, ili kuyataifisha.

Waziri Nchemba amesema hay oleo Jumatatu Machi 26, kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Kiinjli la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Pare Usharika wa Masaka, wilayani humo.

Amesema serikali imeanza kuainisha mashamba hayo ya watu binafsi ambao wamekaidi agizo la serikali na kuendeleza kilimo cha dawa za kulevya kinyume cha sheria.

“Tukishamaliza kuyaainisha mashamba yote yanayolima dawa za kulevya, serikali itayataifisha na wamiliki kufungwa jela miaka 30.

“Same ni miongoni mwa wilaya zinazoongoza kwa kilimo cha mirungi, nawashauri ni vema mkaachana na biashara hiyo na kujihusisha na kilimo cha mazao mengine ya biashara na chakula,” amesema Mwigulu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles