23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kupitia upya gharama za matibabu sekta binafsi

AVELINE  KITOMARY -DAR ES SALAAM

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na Watoto,  imesema itaendela kufanya mazungumzo na sekta binafsi za afya ili kuweza kupunguza gharama za matibabu ambayo itawawezesha Watanzania wengi kumudu hospitali zao .

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam katika kongamano la 20 la Sekta binafsi za Afya (APHFTA) na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Kambi,  alisema kuwa sekta hizo lazima ziendeshwe kwa namna inavyotakiwa ili sekta za binafsi na umma ziweze kunufaika.

“Suala la gharama za matibabu  ni jambo ambalo bado tunaendelea  kufanyia kazi lengo letu mwisho wa siku  ni kwamba gharama ziwenafuu na watanzania wengi waweze kutumia na kupata huduma.

“Hili sio la muda mfupi ni jambo ambalo unatakiwa ukae chini kuliangalia kwa kina kwasababu upande mwingine unataka kukuza sekta binafsi iimarike lakini unapande mwingine unataka watu wengi wapate acceses za huduma zao tutaendelea kujadiliana sisi kama wizara tuko karibu sana na sekta binafsi tunaendelea kuzungumzia changamoto zinazotolewa na sekta binafsi za afya,” alifafanua Prof Kambi.

Pamoja na hali hiyo alizitaka sekta binafsi za afya kufuata maadili na taaluma ya tasnia ya huduma za afya ili kutoa huduma nzuri zaidi kwa jamii.

“Tunazo sera na sheria ambazo zinalinda sekta hizi hivyo biashara hii lazima ifanyike kwa namna inavyotakiwa ili tunufaike wote , sheria lazima zifatwe ulipaji wa kodi  na kuepuka rushwa kwani Rais (John Magufuli),  anaumia anapoona mtanzania anateswa hasa mtanzania maskini.

“Hakikisheni katika vityuo vyenu utoaji wa huduma unazingatia maadili ili watu wapate huduma nzuri,kwenye kodi mambo mengi tumeshafanya yawe rahisi tutaendelewa kufanyia kazi changamoto zenu,” alisisitiza.

Prof Kambi pia alitoa wito kwa Watnzania kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ili waweze kupata matibabu ya haraka wanapougua.

 NHIF WALILIA UAMINIFU

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tiba na Huduma za Ufundi wa (NHIF),  Dk. David Mwanesano,  alisema kuwa baadhi ya wahudumu wa afya wasiokuwa waaminifu wamekuwa wakitoa huduma kwa wateja wa bima ya afya bila kuwa na umakini na kusababisha hasara kwa mfuko huo.

Alisema hali hiyo imekuwa ikichelewesha malipo kwa hospitali binafsi kutokana na uhakiki wa muda mrefu ili kubaini ukweli .

“Kuhusu ucheleweshwaji wa fedha kwa kiwango  kikubwa sasa hivi hali imeimarika kwenye utoaji wa fedha lakini pia wakati mwingine unaweza kukuta kuna matatizo ya hapa na pale  kwa mtoa huduma  na wakati mwingine kwa upande wetu

“Kwa watoa  huduma tungependa kuwashauri  kupeleka madai ambayo ni yaukweli  kwasababu anapopeleka madai ambayo sio ya ukweli  hii inasababisha hasara  na hii ni uvunjifu wa maadili

“Watoa huduma waangalie na  kukagua kwa kina ili wanapoleta  kwetu tuwe na muda mfupi wa kuangali lasivyo tunachukua muda kwasababu hizi ni fedha za umma hatuwezi kulipa bila kukagua,” alisema.

Alitoa wito kwa wahudumu wa afya kuwa waangalifu katika ukaguzi wa kadi za bima ili kubaini waginjwa ambao ni wadanganyifu.

“Niwaombe watoa huduma wote wa binafsi na umma kuwa wahakikishe wanafanya ukaguzi  kwa wagonjwa anapokuja na kadi lazima ahakikishe je huyu ni mwanachama wetu kweli,” alisema Mwanesano

Kwa upande wake Mkurugenzi APHFTA,  Dk. Samwel Ongillo, alisema Sasa wanaangali na kubadilisha muundo wa chama kwa kuwa na kitengo maalumu cha kujiendesha chenyewe kwa ajili ya kupata mapato ya ziada na pia kutoa huduma za kijamii.

“Chama sasa hivi ina karibia wanachama katika  vituo 1000 na tunataka vituo vyote viwe wanachama ambavyo ni sawa na vituo halali 1,800 kwa hiyo tunafanya mikakati ya  kufikia watoa huduma wote binafsi nchini

“Lakini pia kumekuwa na ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi kwa sasa katika kipindi cha mwaka mmoja  na nusu kumekuwa na ongezeko la vituo vya afya binafsi 488 vimesajiliwa kwa kipindi cha miezi 18 haijawahi kutokea kwahiyo sekta inakua  kwa kasi,” alisema Dk. Ogillo.

Aidha alikemea vitendo ambavyo ni kinyume na maadili katika vituo hivyo na kuwataka wanachama kufata miongozo ya taaluma yao.

“Chama chetu ni cha watu ambao ni waaminifu na mtu kama sio  mwaminifu au ameleta utapeli  huyo hafai kuwa  mwanachama kwa sababu katiba inasema mwanachama  mwanaminifu anatakiwa kufata sheria za nchi pamoja mipango iliyokubalika,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles