27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI KUPIGA MARUFUKU MADINI FEKI

NA JANETH MUSHI-ARUSHA


SERIKALI imejipanga kuzuia uuzwaji wa madini feki aina ya Tanzanite kwenye  maonesho na minada  ya madini ya vito.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Benjamini Mchwampaka, alipokuwa akizungumza katika Maonesho ya Sita ya Madini ya Vito yanayoendelea jijini hapa.

Alisema kuwa katika baadhi ya maonyesho kumekuwa na tabia ya baadhi ya wauzaji kuuza madini feki hivyo wamejipanga kuwachukulia hatua za kisheria.

"Katika minada mingine kumekuwa na baadhi ya wauzaji wanauza madini feki, hatutaki hili litokee hapa,wanunuzi msijali kwani kuna maabara hapa unaweza kupimiwa madini kabla haujauziwa na sheria zitachukuliwa kwa watakaobainika," alisema.

Kwa upande wake Kaimu  Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe,alisema katika maonyesho hayo Kampuni  ya Tanzanite  One inatarajia kuuza madini katika mnada utakaofanyika kwenye maonyesho hayo.

Alisema hiyo ni kampuni pekee iliyojitokeza kuuza madini yake katika mnada na kuwataka wauzaji wadogo kutumia fursa hiyo kujitangaza kwa wanunuzi kutoka nje ya nchi wanaoshiriki maonyesho hayo.

 Akizungumzia uuzaji wa madini feki, alisema kuwa atakayekamatwa nayo hatua ya kwanza yatataifishwa na kamishna wa madini kwa mujibu wa sheria na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Alitaja nchi zilizoshiriki kununua madini hayo ni pamoja na Kenya, India, Marekani, Sudan, Malawi, Canada, Swaziland, Afrika Kusini, Israel, Italy ambapo alisema hiyo ni fursa kubwa kiuchumi ya kuwaunganisha wachimbaji wakubwa,wakati na wadogo katika biashara hiyo.

Awali mgeni rasmi katika maonesho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bandera aliwataka wachimbaji wadogo wa madini hayo kuyaongezea thamani kwa kuyachakata ili kuweza kukuza mitaji yao.

Alisema kuwa madini hayo hayapatikani maeneo mengine bali Tanzania pekee hivyo ni vyema yakaongezwa thamani ikiwemo kupatikana kwa soko la uhakika ili kila mwananchi aweze kuyanunua badala ya wageni kutoka nchi nyingine kuyanunua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles