26 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kupanga bei linganishi ya mafuta

Na Mwandishi wetu,Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Nishati imepanga kuweka bei linganifu ya mafuta ya taa, petroli na dizeli ili kuondoa utofauti uliopo kati ya mkoa mmoja hadi mwingine katika ununuzi wa mafuta.

Kauli hiyo imetolewa leo Januari 30,2024 na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo kuhusu majukumu, mafanikio na changamoto za Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Judith amesema lengo nikuwasaidia wananchi waishio mikoa ya pembezoni kupata bidhaa hiyo kwa bei nafuu.

Ameeleza kuwa serikali imeanza kuwekeza kwenye mifumo ya kieletroniki ikiwemo ujenzi wa miundombinu mipya ya kisasa katika maeneo tofauti nchini ili kufanikiwa kupanga bei linganifu.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo, Dk. Jasson Rweikiza ameipongeza serikali kwa kuanza utaratibu wa kupanga bei linganishi ya mafuta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles