29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

SERIKALI KUMWAGA AJIRA 52,436

Na ELIZABETH HOMBO

-DODOMA

SERIKALI inakusudia kuajiri watumishi wapya 52,436 katika mwaka ujao wa fedha.

Ajira hizo mpya ni tofauti na zile za madaktari 258 na wataalamu wa afya 11 waliotangazwa kuajiriwa Jumatano wiki hii baada ya kupeleka maombi na kukidhi vigezo kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya kwenda kufanya kazi nchini Kenya.

Akizungumza bungeni juzi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, wakati alipofanya majumuisho ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha wa 2017/2018 alisema:

“Tunatambua umuhimu wa rasilimali watu wanaotosheleza, kama nilivyoeleza wakati nasoma bajeti kuwa tulishatoa vibali 9,700 vya ajira na tayari wameshaingia kazini.

“Namshukuru rais kwa kuona umuhimu wa kuajiri madaktari 258 na kwamba Jumatatu wanaanza kazi rasmi,” alisema.

Alisema wataendelea kuajiri kwa awamu na watahakikisha kwamba hawarudii makosa yaliyotokea ikiwamo ya watumishi hewa.

Pia alisema zaidi ya maofisa 1,595 waliosababisha kuwapo kwa watumishi hewa 19,708 wamechukuliwa hatua na kwamba wengine wana kesi mahakamani.

Alisema watumishi hao hewa  walibainika wakati wa uhakiki katika orodha ya malipo ya mishahara, hivyo waliondolewa na kama wangeachwa wangeigharimu Serikali Sh bilioni 19.8 kwa mwezi.

“Kumekuwa na malalamiko kuwa Serikali hii ni ya kuhakiki tu. Naomba niwaeleze kuwa hatuwezi kukaa na watumishi bila kujua kila mmoja ana sifa zipi na weledi au anatekeleza wajibu wake kwa kiasi gani.

“Tutaendelea na mpango huu wa uhakiki na kwamba ni endelevu na tutaendelea kufanya hivyo na wala hatutishwi na maneno ya watu.

“Kupitia uhakiki tuliofanya watumishi zaidi ya 19,708 wamebainika katika orodha ya malipo yetu ya mishahara na waliondolewa, tungewaacha wangeigharimu Serikali kwa mwezi shilingi bilioni 19.8.

“Maofisa zaidi ya 1,595 wa madaraka mbalimbali walioshiriki kuwepo kwa watumishi hao hewa tumewachukulia hatua na kwamba wengine wana kesi mahakamani na tayari shilingi bilioni 9.3 zimesharudishwa hazina,” alisema.

 

Angellah alisema Serikali ilifanya uamuzi wa uhakiki kwa nia njema na itatenga fedha ili kukamilisha mchakato wa utambuzi na uandikishaji.

Aliwataka waajiri wote nchini kuweka kipaumbele katika kuandaa umuhimu wa mafunzo kwa watumishi wao.

Alisema kwa mwaka wa fedha 2015/2016 watumishi 395 walipatiwa mafunzo nje ya nchi na katika mwaka wa fedha 2017/2018, watumishi wa umma 654 nao walipatiwa mafunzo. 

“Tunayo sera ya mafunzo ambayo inasisitiza waajiri kuweka vipaumbele katika kuandaa umuhimu wa mafunzo kwa watumishi wao ambayo itazingatia mahitaji yao halisi. Kupitia ofisi yangu idara ya rasilimali watu wamekuwa wakitafuta fursa ya mafunzo nje ya nchi ili kuhakikisha watumishi wengi zaidi wanaweza kujiendeleza.

“Natoa rai kwa waajiri kama ambavyo wanatenga fedha kwa kuzingatia masuala mbalimbali, ni vyema katika bajeti zao wayape kipaumbele mafunzo kwa watumishi wao. Tusitafute visingizio eti kwa sababu hakuna fedha,” alisema.

SIMBACHAWENE

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene, alisema kwa mwaka ujao wa fedha wa 2017/2018, Serikali imetenga Sh bilioni 96.3 kwa ajili ya kununua dawa.

Alisema kumekuwa na upungufu wa watumishi 96,000 huku waliopo wakiwa ni 46,000.

Kuhusu madeni ya walimu, alisema madeni yote ambayo si ya mshahara wameshayalipa.

Akijibu hoja za wabunge kuhusu kuwapo migongano ya uongozi inayosababishwa na wakuu wa mikoa na wilaya alisema:

“Kwanza hao wanaotajwa wapo kwa mujibu wa sheria hivyo hakuna namna lazima waelewane.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles