30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kukiongezea uwezo kiwanda cha nyama Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Geoffrey Mwambe, amesema Serikali imedhamiria kuufanya uwekezaji wa kiwanda cha kusindika nyama cha SAAFI  kilichopo Sumbawanga ili kiweze kufanya uzalishaji mkubwa kulingana na uwezo mitambo na mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

Mwambe aliyeambatana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki, amesema serikali itachambua kwa kina uwekezaji wa kiwanda hicho, lengo kujua  namna ya kukiwezesha ili kuzalisha kwa ufanisi.

“Nimeabiwa kiwanda hiki masoko ndani ya Afrika kwa nchi za Comoro, Zambia na nje ya Afrika  kama Dubai. Kiwanda hiki kitaongeza faida kwa Wanasumbawanga, kwa vijana kupata ajira, wafugaji kupata soko la mifugo yao pamoja na nchi itapata fedha za kigeni kwa kuuza nyama nje ya nchi,” amesema Mwambe.

Amebainisha kuwa uwekezaji katika Mkoa wa Rukwa ni muhimu  kutokana na mkoa huo upo kwenye lango la soko la SADC.

Aidha, amefafanua kuwa kwa kulitambua hilo, serikali imetenga fedha katika bajeti ya mwaka huu za kujenga uwanja wa ndege mjini Sumbawanga. 

Kwa upande wake Ndaki, amefafanua kuwa kiwanda hicho kikiwezeshwa kuzalisha kwa ufanisi kitaweza kuwasaidia wafugaji wa mkoa huo kupata soko la uhakika la mifugo yao na kuongeza kipato.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SAAFI, Theresia Mzindakaya, ameishukuru serikali kwa nia yake ya kuendelea kuwasaidia ya kuhakikisha kiwanda hicho kinazalisha  kwa kiwango cha malengo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles