23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

SERIKALI KUHAKIKI VIASHIRIA UPUNGUFU WA CHAKULA

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Wizara ya Kilimo imesema itaendelea kufuatilia kwa karibu wilaya zote zenye viashiria vya upungufu wa chakula na kuhakikisha upatikanaji wa chakula.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Joyce Solombi (CCM), Naibu Waziri wa Kilimo Dk. Mary Mwanjelwa amesema ufuatiliaji huo ni pamoja na kufanya tathimini ya kina ya chakula na lishe.

Katika swali lake Joyce alitakakujua serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wananchi wa Wilaya ya Serengeti na Bunda wanaoshi kandokando ya Mbuga ya Serengeti ambao mazao yao yameathiriwa na wanayapori wakiwamo tembo.

“Tathmini hiyo itaanishisha hali halisi ya upatikanaji wa chakula, idadi ya watu walioathirika, viwango vya athari, kipindi cha athari na sababu zilizosababisha kisha baada ya tathmini hiyo hatua stahiki zitachukuliwa na serikali na wadau wengine katika kipindi cha muda mfupi,” amsema Dk. Mwanjelwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles