Serikali kugawa mabehewa kwa wafanyabishara wa bandari

0
501

Na MWANDISHI WETU -KAGERA

SERIKALI imesema ipo tayari kugawa mabehewa kwa wafanyabiashara ili waweze kusafirisha mizigo yao kwa kwa treni na meli kama njia ya kuimarisha sekta ya uchukuzi kupitia usafiri huo.

Kutokana na mkakati huo imesema watagawa mabehewa zaidi ya 1,000  yanayomilikiwa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa wafanyabiashara wakubwa ambao watayahitaji kwa ajili ya kusafirisha mizigo yao kutoka bandarini kwenda sehemu mbalimbali nchini.

Akizungumza jana katika Bandari ya Bukoba na baadaye  Kemondo Bay zilizopo mkoani Kagera, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, alisema mchakato huo wa kutoa mabehewa utaanza baada ya kufanyika kikao kati yake na wadau wakiwamo wafanyabishara wanaotumia usafiri wa meli na reli kwa ajili ya kusafirisha mizigo yao.

Kamwelwe, alisema mabehewa hayo watakayopewa wafanyabishara hao wanaohitaji na kuyafanyia matengenezo kwa fedha zao, yatabaki kuwa mali ya TRC.

“Mabehewa ambayo tunayo pale TRC tutawapa wafanamyabiashara na sisi tutawaruhsu kutumia miundombinu ya reli lakini tutakuwa tukipata ushuru unaotokana na kutumia reli.

“Hivyo kati ya siku mbili hizi nitakuwa na kikao na Mkurugenzi wa TRC,  Mhandisi Masanja Kadogosa ili kujadili kwa kina suala hilo ambalo sasa litatufanya turahisishe utoaji wa huduma za usafiri, tunaka tukimbie kwani tumechelewesha sana,” alisema Kamwelwe.

Bandari ya Bukoba

Akiwa katika Bandari ya Bukoba, Kamwelwe, alisema ilianza kujengwa mwaka 1943 na kukamilika mwaka 1945 ambapo wakati huo ilianza kutumia kwa vyombo mbalimbali vya majini lakini baadaye Serikali ikawa na meli zake ikiwamo za Mv Bukoba, MV Victoria na MV Butiama. 

 “Mv Victoria kwa bahati mbaya ilizama lakini pia tulikuwa na meli nyingine Mv Clarias iliharibika. Lakini baada ya kuanza awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli, ambaye amekuwa na dhamira thabiti ya kusubutu, ametoa maelekezo ndio mnaona haya maendeleo sasa bandari hii inakarabatiwa ili iwe mpya. 

“Kinachofanyika ni pamoja na kukarabati magati kwa ajili ya meli ili ziweze kufika sehemu na kupaki lakini pia maghala kwa ajili ya mizigo, chumba cha abiria ambao wanasubiri kusafiri, ofisi za wafanyakazi wa TPA, Kampuni ya Meli Tanzania na TASAC,” alisema 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here