22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali kuendelea kushirikiana na wadau kutoa elimu ya Saratani

Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Serikali imesema itaendelea kushirikiana kwa karibu na wadau na asasi mbalimbali za afya ili kutoa elimu ya ugonjwa wa saratani kwa lengo la kugundulika katika hatua za awali.

Hatua hiyo inakuja baada ya kuendelea kuongezeka kwa ugonjwa wa saratani nchini ambapo jamii imetakiwa kuepuka vihatarishi/ vichocheo ikiwemo matumizi ya tumbaku, unywaji pombe kupindukia, u laji mbaya na kutofanya mazoezi.

Akizungumza Dar es Salaam, katika hafla ya Uzinduzi wa Kitabu cha ‘Ujue Ugonjwa Wa Saratani’ kilichoandikwa na Daktari Bingwa wa Saratani Hellen Makwania, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Aifelo Sichalwe amesema endapo saratani itagundulika katika hatua za awali mgonjwa anaweza kupona.

“Lengo letu ni jamii kugundua ugonjwa huu katika hatua za awali utoaji wa elimu ya ugunduzi wa saratani katika hatua ya awali ni suala ambalo linatiliwa mkazo zaidi na ni mkakati wa magonjwa yasiyoambukiza ili watu waweze kuchukua hatua mapema.

“Ndugu zangu ni lazima tuweke utaratibu wa kufanya mazoezi,kuepuka unywaji pombe kupindukia na matumizi ya tumbaku na sigara ni vichocheo vya magonjwa yasiyoambukiza,” amesema Dk. Sichalwe.

Dk Sichalwe alisema tafiti za Mashirika ya Umoja wa Mataifa za mwaka 2018 za takwimu za saratania Wagonjwa wanaongezeka siku hadi siku huku kwa kila watu 100,000 kuna wagonjwa 76 kila mwaka.

“Na hii ni sawa na makadirio ya wagonjwa wapya wa saratani 42,060 kwa mwaka na huku taarifa za vifo zikibainisha wagonjwa 28,610 hufarikia swa na asilimia 68 ya wagonjwa wapya hufariki.

“Takwimu za kanzi data za hospitali zetu za Kanda za mwaka 2000 zinaonesha kwamba wagonjwa wapya 12,096 waligundulika ambao ni sawa na asilimia 28 ya wagonjwa wapya wote kwa mwaka 2010 ikilinganishwa na wagonjwa halisi waliofikiwa.

“Kanda ya Mashariki wagonjwa waliobainika ni 7,381, Kanda ya
Ziwa 1,098 na kanda ya kaskazini 2,083, takwimu hizi ni kubwa na tunatakiwa kuchungua hatua stahiki ,”amesema.

Amesema Serikali inaendelea kuboresha miongozi ili wazee kurudi katika jamii iwe ni kitu muhimu ili kutoa elimu ya saratani.

Ametoa Wito kwa wahudumu wa afya kutumia taaluma zao kutoa elimu kwa jamii kwa njia mbalimbali ili jamii inufaike na elimu yao.

“Kila mtu anatakiwa kushirika katika kupambana na magonjwa haya kwani ni ya gharama kubwa na pia rasilimali za watu sio nyingi ni wajibu wetu kutoa elimu kila mtu kwa nafasi yake.

Kwa upande wake, Dk. Makwani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi inayojihusisha ma masuala ya saratani cha Genesis For Palliative Care Service Foundation alisema tangu atoe kitabu cha kwanza mwaka 2019 kimewafakia jamii hadi maeneo ya vijijini.

“Nilipata mrejesho kutoka kwa watu 18 waliokisoma kitabu kati ya hao 13 walikutwa na ugonjwa walitibiwa na kupona, watano waligundulika katika hatua ya juu na walifarikia.

“Naamini kuwa kitabu hiki kilichoandikwa kwa lugha ya kiswahili kitasaidia watu wengi kupata uelewa kuhusu ugonjwa huo na kupata matibabu mapema,”amesema Dk Makwani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles