27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali kuboresha miundombinu ya bandari

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Joseph Nyamuhanga.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Joseph Nyamuhanga.

Na Amina Omari, Pangani

SERIKALI imejipanga kuhakikisha inafanya maboresho katika bandari zake zote kwa kujenga miundombinu ya kisasa ili kuhakikisha wanaimarisha shughuli za usafirishaji ili kufikia ndoto ya uchumi wa kati.

Ahadi hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Joseph Nyamuhanga, wakati wa ufunguzi wa kivuko cha MV Pangani pamoja na gati, uliofanyika wilayani Pangani juzi.

Alisema tayari timu ya wahandisi imeanza kufanya tathmini ya changamoto za uhaba wa vifaa zinazozikabili bandari zote ili kubaini upungufu uliopo.

“Licha ya kubaini, wahandisi hawa watakuwa na jukumu la kuainisha mahitaji rasmi yaliyoko kwenye Bandari zetu na kisha kuandika mapendekezo ili serikali iweze kuyafanyia kazi kwa haraka,” alisema Katibu Mkuu huyo.

Kwa upande wa gati la Pangani, alisema imegharimu Sh bilioni 3.1, fedha zilizotokana na mapato ya ndani.

Alisema kukamilika kwa gati hiyo kutawezesha shughuli za usafirishaji wa shehena za mizigo kwa urahisi, hivyo kuondoa changamoto zilizokuwepo hapo awali.

Kwa upande wa kivuko, alisema kimeweza kugharimu Sh bilioni 4 na kitasaidia kumaliza changamoto ya usafiri katika eneo hilo.

Nao baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo, waliishukuru Serikali kwa kuweza kutimiza ahadi zake katika kipindi kifupi cha uongozi wa Rais Dk. John Magufuli.

Mmoja wa wananchi hao, Mohammed Ahmed, alisema kivuko hicho cha kisasa kitarahisisha usafiri badala ya kusubiri kivuko kimoja, kwani sasa vitakuwepo viwili vinafanya kazi.

“Hili la kivuko tunashukuru kutokana na kupata gati mpya, Serikali ione namna ya kuleta usafiri wa uhakika wa meli kutoka Tanga hadi Unguja ili tuweze kusafirisha bidhaa zetu kwa urahisi,” alishauri Ahmed.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles