28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali kuanza kutekeleza mradi mkubwa wa kufua umeme mto Malagarasi

Na Editha Karlo, Kigoma

Serikali imeanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa kufua umeme katika mto Malagarasi mkoani Kigoma kwa Kutangaza zabuni yenye gharama ya zaidi ya Sh bilioni 400 ambao unatajwa utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha Megawat za umeme 49.5.

Hayo yamebainishwa juzi na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Stephen Manda wakati wakikagua eneo la utekelezaji wa mradi huo ambapo amesema Mkandarasi ambaye atashinda zabuni atatakiwa kutekeleza mradi huo kwa muda wa miaka tatu na miezi sita.

Mhandisi Manda amesema serikali imeiangalia Kigoma kwa jicho la kipekee katika uboreshaji wa miundombinu ya nishati ya umeme ili wakazi wa mkoa wa Kigoma waondokane na matumzi ya umeme wa mafuta.

“Mradi huu unahusisha ujenzi wa bwawa na jengo la mtambo, kituo cha kupokea umeme na kusafirisha pamoja njia ya kusafirisha msongo wenye km132 kutoka malagarasi kwenda Kidahwe,” amefafanua Mhandisi Manda.

Kwa upande wake Meneja mradi huo, Mhandisi Victor Rutina amesema mradi wa umeme utakwenda sambamba na ujenzi wa barabara kiwango cha lami chenye kilometa 22 kutoka kwenye eneo la mradi mpaka barabara kuu.

Baadhi ya wakazi wanaoishi karibia na mto wa Malagarasi wamepokea mradi vizuri kwani kumekuwa na changamoto ya umeme pamoja na barabara na kuamini kuwa watanufaika zaidi kwa kusafirisha mazao yao pamoja na wagonjwa kwa urahisi.

“Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wetu mpendwa Samia Suluhu kwa kuiona hii changamoto iliyo kuwa inatukabili ya kuwa na umeme ambapo mradi huu utaenda sambamba na ujenzi wa barabara ya uhakika hii itatusaidia sana katika kutekeleza majukumu yetu mbalimbali ya kijamii, mradi tumeupokea vizuri,” amesema mmoja wa wakazi wa eneo la Malagarasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles