22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Serikali itoe msamaha wa kodi kwa wawekezaji binafsi

filbert-bayiNa WINFRIDA NGONYANI-DAR ES SALAAM.

SERIKALI imetakiwa kuwatia moyo wawekezaji binafsi katika vituo na shule za michezo kwa kutoa msamaha wa kodi na ushuru wa vifaa vinavyohusu michezo mashuleni na katika vituo vinavyokuza maendeleo ya michezo.

Hilo ni moja ya pendekezo lililowasilishwa Serikalini na wadau wa michezo mbalimbali waliokutana hivi karibuni mjini Kibaha, Pwani, kujadili kushuka kwa maendeleo ya michezo nchini.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi, alisema tayari wamewasilisha mapendekezo kadhaa Serikalini yatakayoingizwa katika sera mpya ya michezo.

Alisema wadau wamependekeza kuwa kutokana na shule, vyuo na vituo vya michezo nchini kutotumika kikamilifu kuchangia ukuaji wa michezo na uwezo wa kushinda katika michezo ya mashindano, ni wakati mwafaka wa kufanya uamuzi wa kuvitumia.

“Vyuo vya mafunzo ya walimu wa michezo kama vile Malya na Butimba, vipewe jukumu la msingi la kimkakati la kuzalisha walimu wa michezo mashuleni na katika vilabu vya michezo, viboreshwe ikiwezekana viongezwe na kupangwa kwa kanda,” alisema.

 Alisema wadau pia wameishauri Serikali ihamasishe kuwepo kwa somo la elimu ya masoko katika michezo (Sports Marketing), kwenye vyuo vya michezo.

“Timu na vyama vyetu vya michezo havijaweza kufanikiwa kutumia masoko katika michezo kwa faida inayostahili, hii inatokana na uelewa na utaalamu mdogo katika nyanja za masoko katika michezo,  Tanzania inayo wataalamu wachache sana katika eneo la masoko katika michezo.

“Kama nchi tunaweza kufanikiwa kuifikisha michezo kwenye manufaa makubwa bila kutegemea fedha za Serikali endapo tutawekeza kuwa na wataalamu na kuwatumia wataalamu wa masoko katika michezo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles