24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 25, 2022

Serikali itaendelea kuwasaidia wakulima wa pamba- Bashe

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Serikali itaendelea kuhakikisha inawasaidia wakulima wa zao la pamba kwa kuhakikisha wanapata maslahi mazuri.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini hapa wakati akifanya majumuisho ya majadiliano ya wadau wa zao la Pamba na Bodi ya zao hilo.

Kikao hicho kiliongozwa na Waziri wa Kilimo,Profesa Adolf Mkenda na kuhudhuriwa na Wakuu wa Mikoa ambao Mikoa yao inalima zao la Pamba.

Naibu Waziri Bashe alisema mojawapo ya wajibu wa Wizara hiyo ni kuhakikisha inalinda maslahi ya wakulima na wanunuzi.

Alisema ndio maana waliziomba Taasisi za fedha ziendelee kutoa fedha kwa ajili ya wakulima ambapo alidai zoezi hilo limefanyika vizuri na wakulima wanaendelea kunufaika.

Alisema amepambana kuhakikisha ushirika unakaa vizuri japo akakiri kwamba bado kuna wapiga dili.

“Ushirika ulikuwa hauaminiki kabisa,sasa hivi afadhali japo kuna wapiga dili bado wapo.Kikubwa Serikali inalipa kipaumbele zao la Pamba,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,160FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles