SERIKALI IMEZITAKA TAASISI ZOTE KUJIUNGA KATIKA MATUMIZI YA KITUO CHA TAIFA CHA KUTUNZIA KUMBUKUMBU

0
567
ngonyani-1
Mhandisi Edwin Ngonyani

Serikali  imezitaka taasisi zote  kujiunga katika matumizi  ya  Kituo cha Taifa cha  Kutunzia  Kumbukumbu (Internet Data Center)  ili kupunguza  gharama kubwa  za utunzwaji  wa ‘data’ wanazolipia nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, lengo la kujenga kituo hicho ni kutunza ‘data’ nchini kwani ni salama zaidi kuliko nje ya nchi ambapo  baadhi ya watu wasio waaminifu wanaweza kusambaza data zako bila wewe kujua.

“Kutokana na kuwepo kwa kituo hiki kutakuwa na gharama ndogo za  kulipia  huduma ikiwa tofauti na nje ya nchi ambako wanalipia gharama kubwa kutasaidia kuongeza pato la Taifa,”alisema Mhandisi Ngonyani.

Alisema  kituo hicho kinauwezo  mkubwa wa kutunza data na kuwa ujenzi wa kituo hicho umegharimu shilingi bilioni 77 na bado gharama  zinaendelea kuongezeka .

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here