23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

SERIKALI IMECHUKUA UAMUZI SASA KURUHUSU MABASI



Serikali imetangaza rasmi kuwa wimbi mbili zinajazo itaruhusu wamiliki wa mabasi kuanza safari zao za kwenda mikoani saa 11 alfajiri.

Uamuzi huu, umekuja baada ya kuwapo  na kilio cha muda mrefu kutoka kwa wamiliki kuwa, muda mwingi umekuwa ukipotea kutokana na ukaguzi unaofanywa katika stendi  kuu ya mabasi Ubungo, Dar es Salaam.

Pamoja na hayo, wamiliki hawapingi ukaguzi, lakini walikuwa wakisitishwa na upotevu wa muda mwingi, kwa mfano basi linatakiwa kuondoa kituoni saa 12:30 asubuhi, lakini kutokana na muda mwingi wa ukaguzi hujikutana linaondoka saa mbili kasoro robo.

Hali hii kwa kweli inakuwa kero kubwa kwa wasafari ambao wanapotoka Dar es Salaam kwenda mikoani, wengi wao hutegemea wafike mapema ili kwenda maeneo ya vijijini au wilaya zingine kulingana na ratiba zao za kazi.

Tunakubaliana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukukizi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye kuwa uamuzi huu ni sahihi utasaidia kuokoa muda mwingi uliokuwa unapotea kituoni hapo.

Ndiyo maana Waziri Nditiye alipofanya ziara kwenye stendi ya Ubungo kujionea halisi alfajiri, alibaini namna wananchi wanavyopata kero hii. Lakini kuwapo msongamano mkubwa wa ukaguzi wa  magari unaofanywa na wakaguzi wachache  kutoka jeshi la polisi.

Kutokana na hali hiyo, alisema hakuna sababu ya kuwazuia wamiliki wa mabasi wanaotaka magari yao yaanze safari alfajiri kwa sababu maeneo mengi ya nchi yako salama kwa sasa.

Alisema kwa kuanza magari ya mikoa ya Mwanza, Mbeya, Arusha na Dodoma yataanza kuondoka  muda huo kwa sababu njia hizo hazina matatizo yoyote ya ujambazi.

Kutokana na hali hiyo, kwanza tunawashauri wamiliki wote wa mabasi kukubaliana na Serikali katika jambo hili na kuweka utaratibu wa ukaguzi wa mabasi haya siku moja kabla ili kuondokana na usumbufu.

Kwa kufanya hivi kuutasaidia kuondoka kituoni kwa wakati uliopangwa. Hatuoni sababu kwanini mabasi yanaytoka Dar es Salaam kwenda Mwanza yalale Shinyanga, wakati hakuna matukio ya ujambazi ambayo yanahatarisha usalama wa abiria.

Hatuamini kama kweli wamiliki walikuwa wanakaidi agizo la kupeleka mabasi yao yakaguliwe siku kabla, inawezekana hakukuwa na kauli kutoka sehemu husika.

Kutokana na hali hii, tunaishauri Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kujipanga vizuri ndani ya wiki mbili hizi  zilizotolewa ili mabasi  yaweza  kufuata ratiba mpya itakayotolewa.

Tunaamini sasa Chama cha wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), wamepokea ujumbe huu kwa mikono miwili maana wamekuwa na kilio cha muda mrefu mno.

Wito wetu kwa TABOA, wahakikishe wanapeleka magari yao kukaguliwa kwa wakati kama ambavyo wametakiwa kufanya ili kuwasaidia Watanzania ambao wanateseka na kuingia gharama kubwa za safari.

Kama wakifanya hivi, watawapunguza abiria wao gharama za kulala ndani ya mabasi na vyumba za kulala wageni kwa sababu safari zao huwa hazifiki mwisho kwa siku moja.

Sisi MTANZANIA, tunasema katika hili pande zote mbili yaani Serikali na wamiliki wanapaswa kushirikiana kwa kila hatua ili kufikia malengo ya kuwahudumia Watanzania.

Tungependa kuona kuona ujio wa ratiba mpya unakuwa na tija ili Watanzania hawa ambao wakati  mwingine wengi hujishughulisha na biashara zao, wawezi kufika maeneo wanayokwenda kwa wakati.

Tunamalizia kwa kusema serikali imechukia hatua sahihi katika jambo hili, tunasubiri utekelezaji wenye tija sasa kwa manufaa ya wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles