22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

‘SERIKALI HUPOTEZA DOLA MIL 100 KWA KUAGIZA DAWA’

Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM

SERIKALI inapoteza dola za Marekani milioni 100 kila mwaka kutokana na kuagiza dawa kutoka nje ya nchi.

Viwanda vya dawa vilivyopo nchini ni 13 tu ambapo uwezo wake wa kuzalisha ni asilimia 20 ya dawa zote zinazohitajika nchini.

Hayo yalisemwa juzi na Mfamasia wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Siana Mapunjo, wakati wa mkutano wa wadau wa mradi wa kiwanda cha dawa za binadamu cha Zinga ambacho kinatarajiwa kujengwa wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Mapunjo alikuwa akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

“Hii ni fursa kwa Kiwanda cha Zinga kusaidia nchi kupata dawa muhimu kwa wakati na kuokoa fedha za kigeni, kuongeza ajira na kuiwezesha Tanzania ya Viwanda kufikiwa,” alisema Mapunjo.

Alisema gharama hizo zinaongezeka kila mwaka na inakadiriwa ifikapo mwaka 2021 zitafikia Dola za Marekani milioni 350 kwa mwaka.

Awali Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Dk. Mary Mayige, alisema ujenzi huo utagharimu zaidi ya Sh bilioni 70 na wanatarajia kutumia teknolojia za kisasa kutoka Ujerumani.

"Dawa zitakazotengenezwa zitakuwa na kiwango cha juu cha ubora kuweza kushindanishwa na dawa zinazotoka kwenye soko la kimataifa," alisema Dk. Mayige.

Alisema kiwanda hicho kitatengeneza dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi (ARVs), antibiotiki, malaria, kisukari, presha, magonjwa ya kuambukiza na zile za magonjwa yasiyoambukiza.

Alisema uzalishaji wa dawa za binadamu nchini bado ni mdogo na upatikanaji wa dawa zinazozalishwa na viwanda vya ndani umeshuka kiwango ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,220FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles