23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali haitavunja nyumba za waliojenga bondeni

Ramadhan Hassan, Dodoma

Bunge limeelezwa kuwa serikali hairuhusu na haitavunja makazi ya watu waliojenga maeneo hatarishi ikiwamo mabondeni.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Alhamisi Mei 30 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti maalumu,  Zainab Amiri (CUF).

Katika swali lake, mbunge huyo alisema kuna baadhi ya watu wanajenga kwenye mabonde, wengine jirani na hifadhi ya barabara na reli lakini serikali hukusanya kodi za maeneo na majengo katika maeneo hayo.

“Je, serikali inaeleza nini kuhusu kadhia hii, ili mwananchi ajenge mahali husika lazima apate kibali, je, nini adhabu ambayo wanapewa wanaotoa vibali kwenye maeneo hatarishi,” alihoji.

Akijibu swali hilo, Waziri Lukuvi amesema utoaji wa leseni za makazi hautafanyika kwa watu waliojenga maeneo hatarishi.

“Ni kweli kuna watu wanajenga kwenye hifadhi za barabara na hifadhi za miundombinu mingine na mabondeni lakini wamefanya hivyo kinyume na sheria, serikali hairuhusu na hata zoezi la urasimishaji na utoaji wa leseni za makazi,” amesema Lukuvi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles