23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

SERIKALI HAITABINAFSISHA KARAFUU- DK SHEIN

dk-ally-mohamed-shein

Na Muhammed Khamis (UoI)

RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, amesema Serikali haikusudii kubinafsisha zao la karafuu visiwani hapa ili kuendelea kulifanya zao hilo kuonekana bora katika soko la kimataifa.

Rais Shein aliyasema hayo jana Mjini Unguja wakati wa uzinduzi wa utambuzi wa bidhaa ya karafuu (branding) inayotoka Zanzibar ambayo itaiwezesha bidhaa hiyo kutambulika kimataifa wapi inapotokea.

Alisema visiwa vya Zanzibar ni miongoni mwa visiwa pekee vilivyopata bahati kuliko maeneo mengine yote ulimwenguni kwa kuzalisha karafuu bora na zenye kiwango cha juu kwenye soko la kimataifa.

Alieleza kuwa Serikali kwa kuliona hilo ndio maana wameendelea kuhakikisha hawatoi nafasi kwa wawekezaji juu ya zao hilo ili kuepusha kuhujumiwa kwa uchumi wa Serikali pamoja na kufanya udanganyifu hatimaye Zanzibar kupoteza nafasi yake kwenye soko la kimataifa dhidi ya zao la karafuu.

Pamoja na hayo Rais Shein aliutaka uongozi wa Shirika la Biashara (ZSTC) kuwa makini na zao hilo ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati imara kwa wakulima sambamba na kuongeza uzalishaji utakaowasaidia wakulima hao kuondokana na usumbufu.

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko, Amina Salim Ali, alisema Serikali kwa sasa inakusudia kupandisha thamani ya zao hilo ili kuwawezesha wakulima kupata kipato bora zaidi.

Pamoja na hayo waziri huyu aliendelea kufafanua miongoni mwa mikakati yao ni kulinda thamani ya zao hilo na hatimaye kubaki kuwa bora katika soko la kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles