24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali haipaswi kuwa hakimu wa Vyombo vya Habari-Makunga

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali kupitia Idara ya Habari Maelezo imeshauriwa kutojipa jukumu la kusimamia na ‘kuhariri’ vyombo vya habari pia mambo yote yanayotokana na tasnia hiyo kwani jambo hilo sio sahihi.

Kauli hiyo imetolewa na Theophil Makunga, Mwenyekiti Mstaafu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), wakati akizungumzia Mabadilio ya Sheria ya Habari katika Kituo cha Televisheni cha Channel Ten leo Agosti 1, 2022.

Amesema, serikali haipaswi kufanya sensa ama kuwa hakimu wa vyombo vya habari na badala yake, jukumu hilo liundiwe Baraza Huru la Vyombo vya Habari ambalo litatumika kusimamia mambo yote yatayohusu tasnia ya habari.

“Serikali kupitia Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo kupewa jukumu la kuangalia maudhui na kazi za habari, sisi tuliona sio sasasawa.

“Maombi yetu ni kwamba, ile (Idara ya Habari Maleelzo) ibadilishwe jukumu lile, badala ya mambo yanayohusu tasnia ya habari kupewa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, lipewe Baraza Huru la Vyombo vya Habari kusimamia,” amesema Makunga.

Ameeleza kuwa, Baraza Huru la Vyombo vya Habari Huru linapaswa kuwa kama mabaraza ya taaluma zingine akitoa mfanbo wa namna Baraza la Madaktari pia Baraza la Wanasheria yanavyoendeshwa.

“Kinapaswa kuwa chombo cha wanataaluma wahusika kinachoendeshwa na waandishi wa habari. Kwa hiyo, matatizo yote yatakayokuwa yanahusu taaluma ya waandishi wa habari, yapitie kule kwenye lile baraza ambalo litakuwa likiendeshwa na waandishi wa habari wenyewe.

Hata hivyo, Makunga ameipongeza serikali kwa kufungua mlango wa majadiliano kuhusu mabadilio ya sheria zinazoongoza tasnia ya habari nchini.

Kwenye kipindi hicho, Makunga amesema serikali imeona umuhimu wa kufungua mjadala wa mazungumzo ya sheria hizo, kutokana na wadau wa habari kueleza kuwepo haja ya kuzipitia upya.

Tayari serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imeandaa mkutano wa wadau wa habari utakaofanyika kwa siku mbili (tarehe 11 – 12 Agosti 2022).

“Kuna vipengele vinatubana, tunaishukuru serikali kwa kukubali kufungua mjadala wa mazungumzo yanayolenga kuangalia namna gani ya kuondoa hivyo vipengele ili tuwe huru zaidi,” amesema Makunga.

Akizungumzia historia ya sheria ya vyombo vya habari nchini, Makunga amesema tangu awali, vyombo vya habari vilikuwa vikiendeshwa kwa sheria iliyoundwa mwaka 1979 – Sheria ya Magazeti.

“Sheria hii ilikuwa ikiongoza uandishi wa habari, utangazaji na namna gani ya kufanya, ilikuwa inasema ukiwa na kosa kwenye gazeti, anaweza kushtakiwa mwandishi, mhariri, mmiliki, mchapaji wa gazeti,” amesema.

Hata hivyo anasema, kutokana na mabadiliko ya teknolojia, sheria sasa inapaswa kuendanani na wakati uliopo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles