31.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali, Gain yachimba visima 10 vya Lindi

Hadija Omary, Lindi

Serikali ya Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Global Aid Network Tanzania (GAiN), wamechimba visima 10 vya maji  vyenye thamani ya Sh milioni 129.119.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Mkongea Ally,  Kaimu Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Nachingwea Injinia Sultan Ndoliwa, amesema mradi huo ulianza Januari 29, mwaka huu na utakamilika Desemba 30, mwaka huu.

“Mradi huu ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 80 na unatarajiwa kuhudumia jumla ya Wananchi 2,500 katika vijiji 10 sawa na wanufaika 250 kwa siku,” amesema.

Aidha,  Ndoliwa amevitaja vijiji vitakavyonufaika na mradi huo kuwa ni pamoja na Kijiji cha Ikungu, Rupota, Nammanja, Mbondo, Mitugulu, Mtua, Ngumbu, Namatumbusi, Namikongo B na Mapochelo.

Kwa upande wake Mkongea amesema  ameridhika na taarifa za mradi huo, ambapo amewashauri wataalamu wanaohusika na mradi huo kuhakukisha wanatumia vipimo vya kimaabara kwa kila hatua inayofikia ili kuhakikisha maji yanayopatikana yanakuwa salama kwa matumizi.

“Wananchi watakaotumia maji hayo kwa matumizi ya kunywa wahakikishe wanayachemsha kabla ya kuyatumia ili kuua vijidudu ambavyo vinaweza kuleta madhara kwa afya zao,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amewaasa wanachi kutunza miundombinu hiyo ya maji ili iweze kutumika kwa muda mrefu pamoja na kutunza vyanzo vyake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles