28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali: Bei za vyakula kushuka kuanzia Machi

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Serikali imesema kuwa bei za vyakula nchini zitashuka kuanzia mwezi Machi hadi Aprili, mwaka huu kutokana na wingi wa vyakula hatua itakayopunguza makali kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma leo Januari 10, 2023 na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu mikakati ya wizara hiyo ya sasa na ya baadae.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.

“Kama waziri naweza kusema kwamba bei ya chakula itashuka kuanzia mwezi Machi hadi Aprili, mwaka huu kwani vyakula vitakuwa vingi.

“Hivyo, nikiri kwamba ni kweli tuna changamoto ya bei lakini ni kipindi cha mpito tu na baadae bei itashuka. Siyo kwamba wizara ya kilimo hatuelewi upandaji wa bei ya vyakula,” amesema Waziri Bashe.

Amesema serikali imeliona tatizo la kupanda kwa bei ya vyakula sokoni hivyo moja ya mkakati ambao inayo ni kufungua maghala ili kuwarahisishia wananchi katika upatikanaji wa vyakula kwa bei ya vyakula.

Aidha, Bashe ametaja gharama za usafirishaji kuwa ni moja ya sabahu inayochochea kupaa kwa bei ya vyakula nchini nakwamba wanaimani kuwa zitashuka kufikia kipindi hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles