23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali, Airtel zaungana tena

Anna Potinus – Dar es salaam

Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel zimetia saini mkataba wa umiliki wa hisa na makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo ya miezi nane baina ya pande hizo mbili.

Hafla ya utiaji saini imefanyika leo Januari 15, Ikulu jijini Dar es salaam na Rais Dk. John Magufuli ameshuhudia zoezi hilo ambapo Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi ametia saini kwa niaba ya Serikali na Mwenyekiti wa Kampuni ya Bart Airtel Sunil Mittal aemtia saini kwa niaba ya kampuni yake.

Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini makubaliano hayo Rais Magufuli amesema kwa miaka nane Tanzania ilikua haipati gawio kutoka Bhart Airtel ilihali walikuwa na mkataba nao lakini sasa hali hiyo inaenda kubadilika kutokana na makubaliano waliyoingia.

“Miaka yote nane tulikuwa hatupati gawio kutoka Bhart Airtel na ukishaona muda wote huo hatujapata ujue ni biashara mfilisi na ndio maana nilipoingia madarakani tukaliona hili tukasema tuzungumze,” amesema.

Naye Mwenyekiti wa Bharti Airtel Sunil Mittal ameahidi Dola za Kimarekani milioni Moja ambazo Rais Magufuli ameagiza ziende katika ujenzi wa hospitali Dodoma.

“Makao makuu ya Tanzania yako Dodoma tulishaamua fedha tulizoziokoa kutoka sherehe za uhuru na hizi Dola milioni moja kutoka Kwa Mwenyekiti azitoe ziende kwenye ujenzi wa hospitali, tunafanya hivi kusudi ili sikua kifika Dodoma aione hospitali,” amesema Rais Magufuli.

Awali Prof. Kabudi alisema wamefikia makubaliano kuwa Bhart Airtel itakuwa na hisa asilimia 51 kutoka 60  za mwanzo na Serikali itakuwa na hisa asilimia 49 kutoka 40 na nyongeza ya asilimia 9 bila malipo kutoka serikalini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles