30.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 2, 2022

Contact us: [email protected]

SERENGETI BOYS KUTIMUA VUMBI KESHO TAIFA

NA LULU RINGO


Timu ya Taifa chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) inatarajiwa kushuka dimbani kesho kumenyana na Somalia mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo wa kuwania tiketi ya kushiriki mashindano ya mpira wa miguu barani Afrika kwa umri huo yaliyo andaliwa na shirikisho la mpira Afrika ‘CAF’ yamepangwa kufanyika mwakani nchini Tanzania.

Serengeti Boys wameshacheza mchezo mmoja dhidi ya Burundi na kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 ambapo bao la kwanza likifungwa na Kelvin John dakika ya 11 na Agiri Ngoda alifunga bao lapili dakika ya 28 huku Nibikora Arthar akiifungia Burundi goli la kufuta machozi.

Tanzania imepata fursa yakushiriki michuano hiyo kwa kuwa ndiyo mwenyeji hivyo ikiibuka na kombe hilo mshindi wapili wa mashindano hayo ndiyo atapata nafasi ya kushiriki mashindano hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,509FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles