26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Serena, Venus watamba US Open

williams

NEW YORK, MAREKANI

BINGWA wa mchezo wa tenisi duniani kwa upande wa wanawake, Serena Williams na dada yake, Venus William, wameanza vema michuano ya wazi nchini Marekani.

Serena ambaye anashika nafasi ya kwanza kwa ubora kwa upande wa wanawake duniani, ameanza vizuri kwa kumchapa mpinzani wake Ekaterina Makarova, kwa seti 6-3 6-3 katika mchezo huo wa kwanza.

Ushindi huo wa Serena ni wa kwanza tangu atolewe kwenye michuano ya Olimpiki nchini Brazil na alidai alikuwa anasumbuliwa na bega ndio maana alishindwa kufanya vizuri katika michuano hiyo ya Olimpiki, lakini kwa sasa anaendelea vizuri na anaamini atafanya vizuri.

Hata hivyo, baada ya kucheza mchezo huo na kushinda, Serena alisema kuwa ataangalia hali yake ya bega inaendeleaje na kuona kama ataweza kuendelea kucheza michezo ijayo.

Kwa upande wa dada wa Serena, Venus William, naye aliibuka na ushindi katika mchezo wake wa kwanza  kwa kumchapa mpinzani wake Kateryna Kozlova kwa seti mbili, seti ya kwanza akishinda 6-2, akapoteza seti ya pili kwa 5-7, kisha akamaliza kwa ushindi wa 6-4.

Venus alifika hatua ya nusu fainali katika michuano ya Wimbledon miezi miwili iliyopita, lakini alishindwa kufanya vizuri, inaonekana anataka kuzitumia nguvu zake kwenye michuano hii ya wazi nchini Marekani.

“Nashukuru kwa kuanza vizuri katika michuano hii ya wazi, hapa nataka kuonesha uwezo wangu, nilipanga kufanya hivyo kwenye michuano ya Wimbledon lakini niliishia nusu fainali, ila kwenye mchezo huu ninaamini nitafanya vizuri na kutwaa ubingwa.

“Najua ushindani ni mkubwa na watu wamejiandaa vizuri lakini niko tayari kumaliza nguvu zangu kwa ajili ya kuchukua ubingwa wa michuano hiyo,” alisema Venus.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles