27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Serekali kuendelea kuwawezesha wenye ulemavu

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imewahakikishia watu wenye ulemavu kwamba itaendelea kuwawezesha kwa namna mbali mbali ikiwemo kuwapatia elimu ya Usalama na Afya kazini ili kutoa mchango wao kikamilifu katika maendeleo ya nchi.

Kauli hiyo, ilitolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Stella Ikupa, wakati akifungua mafunzo ya usalama na afya yaliyotolewa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa watu wenye ulemavu Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.

Alisema Serikali inatambua mchango mkubwa wa watu wenye ulemavu katika maendeleo ya nchi, kiuchumi na kijamii hivyo itaendelea kuliwezesha kundi hilo kwa kuweka mazingira rafiki ya uzalishaji kupitia taasisi zake.

“Serikali kupitia eaasisi kama  hii na nyinginezo  kwa kushirikiana na wadau mbali mbali kama vile Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA), tutaendelea kuwapa mafunzo mbali mbali yakiwemo mafunzo kuhusu masuala ya usalama na afya kazini,tutaendelea kuwawezesha kiuchumi kwa kuwatafutia masoko ya mazao na bidhaa mnazozalisha na kuhakikisha  kunakuwepo na fursa za uwezeshaji ikiwemo upatikanaji wa mitaji,” alisema.

Aliwakumbusha washiriki wa mafunzo husika kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 kushiriki kuwachagua viongozi wao katika ngazi mbali mbali ambao watawaongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo. 

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda, amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Taasisi yake wa kuyafikia makundi mbali mbali katika jamii na kutoa mafunzo ya Usalama na Afya yatakayowawezesha kufanya shughuli zao kwa kuzingatia kanuni za afya na usalama. 

“Hii sio mara ya kwanza kwa Taasisi yetu kutoa mafunzo kama haya kwa watu wenye ulemavu. Tumeshafanya mafunzo hayo katika mikoa mingine ikiwemo Kagera na Dar es Salaam na kwakuwa ni sehemu ya mkakati wa OSHA basi niwahakikishie kwamba mafunzo haya yatendelea kutolewa katika maeneo mbali mbali ya nchi kwa makundi mbali mbali ya watu,” alisema Mwenda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles