23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Sera za mifuko ya jamii kujadiliwa Dar

samia-suluhuNa Ruth Mnkeni, Dar es Salaam

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassani anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Muungano wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (Pensheni na Afya) na Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Nchi za Afrika Mashariki na Kati (ECASSA).

Hata hivyo nchi wanachama watakaoshiriki katika mkutano huo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Tanzania, Zambia na Sudani ya Kusini.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA), Meshach Bandawe alisema Dar es Salaam jana kuwa dhumuni la mkutano huo ni kujadili sera zinazohusiana na sekta ya jamii.

Alisema mkutano huo utafanyika Februari 18 hadi 19 mwaka huu katika Ukumbi wa Benki Kuu (BoT) ambapo siku ya kwanza washiriki watapokea na kujadili mada mbalimbali za kitaalamu na kutoa mapendekezo yao.

“Siku ya pili itakuwa maalumu kwa mawaziri kuzungumzia hatua zinazochukuliwa na nchi zao ili kupunguza tatizo la ajira. Kwa upande wa Tanzania inapendekezwa itolewe na waziri mmoja kuonyesha hatua za kisera na mipango zinazochukuliwa kukuza ajira na kuboresha hifadhi ya jamii ili kuchangia upunguzaji wa hifadhi,”alisema.

Alisema mkutano huo pia utapokea mada zilizowasilishwa na wataalamu ambapo zitachambuliwa na kuweka maadhimio kwa ajili ya kuboresha sekta ya hifadhi ya jamii katika nchi wanachama.

Aliongeza kuwa kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘Kuainisha Sera za Kiuchumi, Upatikanaji wa Ajira na Maendeleo ya Sekta ya  Hifadhi ya Jamii katika Afrika Mashariki na Kati’.

Aidha alisema washiriki wa mkutano huo watakuwa mawaziri wa sekta zenye dhamana katika mifuko ya hifadhi ya jamii(Pensheni, bima ya afya na fidia kwa wafanyakazi).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles