25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 28, 2023

Contact us: [email protected]

Sengerema kunufaika na usafiri wa majini

MWANDISHI WETU-SENGEREMA

WAKAZI wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, watanufaika na usafiri wa majini baada ya adha ya usafiri huo kwa miaka 61.

Hatua hiyo inatokana na kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa gati la Bandari ya Lushamba uliogharimu Sh bilioni 1.265 ambazo ni fedha za ndani, itakayoanza kutumika Julai mwaka huu baada ya usafiri huo kuwa wa kusuasua tangu mwaka 1958.

Akizungumza na waandishi wa habari katika bandari hiyo iliyopo katika Kijiji cha Kanyala, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Lazaro Mgonzo alisema kuanzia mwaka 1958 hakukuwa na usafiri wa kwenda kisiwani hivyo kuanza kwa usafiri huo utatatua changamoto hiyo.

“Tunashukuru serikali kwa kutukumbuka kwa ujenzi wa bandari ambayo itarahisisha usafiri wa kwenza kisiwani ambao kwa miaka mingi umekuwa na changamoto nyingi,” alisema.

Naye Mtendaji wa kijiji hicho, Benjamin Ndungwizi, alisema licha ya kurahisisha usafiri pia bandari hiyo ambayo inategemewa na wakazi 8,798 wa vitongoji vinne vya Mwibale, Msikitini, Kisarazi na Gembale itatoa ajira kwa vijana wa maeneo hayo kuzunguka kijiji.

“Tunamshukuru Rais John Magufuli kwa kufikiria kutujengea bandari kwa sababu pia ni njia moja ya kututangaza  na sababu nyingine nyingi katika kurahisisha huduma mbalimbali.

“Nitoe wito kwa wananchi kulinda miundombinu ya bandari hii kwa sababu wote ni wanufaika,” alisema.

Awali, Kaimu Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Geofrey Lwesya, alisema mradi huo umefikia asilimia 90 ya kazi ya utekelezaji ambapo sehemu iliyobaki ni kumalizia ujenzi wa jingo la abiria, jingo la mizigo, uzio, vyoo mnara wa tanki la maji na chumba cha mashine ya umeme.

“Ni bandari ndogo, nzuri na ya kisasa kwa sababu imejengwa kwa viwango vya kimataifa, tunategemea wananchi wengi zaidi kuitumia bandari hii,” alisema.

Kwa upande wake Injinia wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Kanda ya Ziwa Victoria, Abraham Msina, alisema gati hilo lina urefu wa mita 60 ambapo wakati wa ujenzi wake nyumba nne za wananchi zililipwa fidia ili kupisha mradi huo.

“Mradi huu ni wa mwaka mmoja ambapo tunategemea mkandarasi kuukabidhi Julai 9, mwaka huu na hatutegemei kuongeza muda,” alisema.

Kwa upande wake mmoja wa wananchi katika Kijiji cha Kanyala, Charles Shuka, alisema wanaishukuru serikali kwa bandari ambapo sasa watatumia meli kulinganisha na boti ambazo zimekuwa ni usafiri hatarishi hiyo lakini pia ifikirie kuwapelekea vivuko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,224FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles