SENETI KUCHAPISHA USHAHIDI UNAOMTUHUMU RAIS TRUMP

0
470

WASHINGTON, MAREKANI


KAMATI ya Bunge la Seneti ya masuala ya usalama nchini hapa inatarajia kuchapisha ushahidi utakaotolewa na James Comey, ambaye amesema Rais Donald Trump alimtaka aache kumchunguza mshauri wake wa zamani wa masuala ya usalama.

Comey ambaye alitimuliwa ukurugenzi wa Shirika la Upelelezi Marekani (FBI), alitoa uchambuzi wa ushahidi wa mazungumzo kati yake na Trump aliyofanya naye mara tano.

Katika mazungumzo hayo, Trump alikuwa akirudia kusisitiza amsikilize na kumheshimu wakati Comey akisisitiza alikuwa akifuata maadili ya kazi yake na bila kuegemea upande wowote.

Maafisa wawili wanaohusika na usalama,Mike Rogers na Dan Coats wamewaambia maseneta kuwa hawakuwahi kulazimishwa kufanya jambo lolote ambalo liko kinyume na sheria.

Lakini wakati wa kikao cha kamati ya Seneti jana Comey alitarajia kueleza kwa kina jinsi Trump alivyosababisha ashikwe na wasi wasi kabla ya kufutwa ukurugenzi wa FBI Mei 9 mwaka huu.

Kamati hiyo ni moja ya majopo pamoja na wizara ya sheria, zikichunguza ripoti za mashirika ya ujasusi ya Marekani kuwa wadukuzi wa Urusi waliingilia uchaguzi wa urais wa Novemba 2016.

Pia kuna uchunguzi unaofuatilia iwapo kundi la kampeni ya Trump lilishirikiana na wadukuzi wa Urusi madai ambayo Urusi imeyakanusha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here