24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Seneta akerwa chama chake kutokuwa na msimamo

WASHINGTON, Marekani

SENETA  wa  Chama cha  Republican, Lisa Murkowski amesema amekerwa na msimamo wa chama chake kabla ya kesi inayomkabili Rais Donald Trump kuwasilishwa  Bunge la Seneti.

Rais Trump, alishtakiwa Bunge la Uwakilishi, linalotawaliwa na wabunge wa Chama cha Democrat kwa utumizi mbaya wa mamlaka na kulizuia Bunge la Congress.

Kwa sasa anakabiliwa na kesi  Bunge la Seneti, linalotawaliwa na wanachama wengi wa Chama cha Republican – ambao wanatakiwa kutopendelea upande mmoja.

Hata hivyo, seneta wa walio wengi katika bunge hilo, Mitch McConnel aliahidi kushirikiana na Ikulu ya Whitihouse.

Trump , ni rais wa tatu kushtakiwa katika mabunge hayo , hatahivyo hakuna uwezekano wa kumuondoa madarakani kutokana na wingi wa Republicans

”Niliposikia hilo nilikerwa sana”, alisema.

Seneta huyo, alisema kunahitajika kuwapo na uwazi na kutoshirikiana kati ya Bunge la Seneti na Ikulu ya Whitehouse kuhusu jinsi kesi hiyo itakavyoandaliwa.

”Kwangu mimi inamaanisha,tunahitaji kurudi nyuma na kutopendelea upande unaojitetea”, alisema. Hatahivyo aliutaja mchakato wote wa kesi hiyo kama ule ulioharakishwa.

 Murkowski , mwanachama wa Republican mwenye msimamo wa kadri , amemkosoa Rais Trump kuhusu sera kadhaa, Oktoba 2018, aliamua kutounga mkono uteuzi wa Trump wa mahakama ya kilele , kufuatia madai ya unyanyasaji wa kingono.

McConnel atachukua jukumu muhimu katika kesi hiyo- ambayo inatarajiwa kutopendelewa -wakati itakapofanywa.

“Huu ni mchakato wa kisiasa. hakuna kinachohusisha mahakama ndani yake . kesi ya kutaka kumuondoa raisi ni uamuzi wa kisiasa”, alisema.

Alisema  alikuwa na matumaini  Rais Trump, ataondolewa mashtaka  Bunge la Seneti, linalodhibitiwa na wanachama wa Republican.

”Tutakuwa na matokeo yatakayopendelea upande mmoja”, alisema.

Democrats wanataka hakikisho na stakhabadhi kuruhusiwa ili kuwezesha kile wanachokitaka kuwa kesi ya haki.

McConell amekataa kuwasilishwa kwa mashahidi ili kutoa ushahidi wakati wa kesi hiyo.

Katika msururu wa jumbe za twitter, rais aliwashutumu wabunge wa Democrats kwa kukataa kuendelea na kesi hiyo kwa kuwa ”kesi yao ilikuwa mbaya”.

Alituma ujumbe wa twitter akisema; Baada ya Democrats kukataa kunipa haki yangu bungeni, bila kuwa na wakili bila mashahidi, sasa wanataka kuliambia bunge la seneti jinsi ya kuendesha kesi hiyo.

”Kwa kweli hawana thibitisho la chochote na  pia hawatakuwepo .Nataka kesi hiyo kufanyika sasa hivi!”

Kwa nini kuna mkwamo kuhusu kuanza kwa kesi hiyo?

Lakini Spika wa Bunge la Uwakilishi, Nancy Pelosi amekataa kufanya hivyo hadi pale sheria za kesi hiyo za seneti zitakapokubaliwa na Democrats.

Kiongozi wa Republican katika Bunge la Seneti, Mitch McConnell, ataamua masharti ya kesi hiyo na Democrats wanamtaka kutoa maelezo kuhusu mashahidi na ushahidi utakaoruhusiwa.

Kuna wabunge 53 wa Republican katika bunge hilo lenye viti 100 na kwa kura hiyo

Kama matokeo ya uchunguzi yaliyopatikana, Democratic kinasema Rais Trump alitoa misaada miwili ya kijeshi yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 400 ambazo tayari zilikuwa zimeshapangwa na bunge na mkutano na Rais Volodymyr Zelensky.

Uchunguzi wa kwanza ambao Rais Trump, aliutaka kutoka kwa Ukraine ulikuwa unahusu makamu wa rais mstaafu Joe Biden, ambaye ni mpinzani wake mkubwa kutoka chama cha Democratic na mtoto wake Hunter.

Ni viongozi wachache wa Marekani ndio walifikia katika hatua ya namna hii. Kwa kuwa chama cha upinzani cha Democratic kina wingi wa wawabunge, kuna uwezekano kuwa Trump ataondolewa mashtaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles