23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

Sekta zinazoongoza kutumikisha watoto zatajwa

Dk. Abdallah Possi
Dk. Abdallah Possi

NA  CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM

UTAFITI wa utumikishwaji watoto wa mwaka 2014 umebaini  watoto milioni tano nchini wanatumikishwa katika  sekta za kilimo, misitu na uvuvi.

Miongoni mwa watoto hao, wavulana ni asilimia 52.5 na wasichana ni asilimia 47.5.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Dk. Abdallah Possi, alikuwa akizungumza   Dar es Salaam juzi katika uzinduzi wa ripoti hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) , Serikali na Shirika la Kazi Duniani (ILO).

Alisema katika utafiti huo,  imebainika ongezeko la watoto hao wanaotumikishwa limeshuka kutoka asilimia 31.1 kwa mwaka 2006 hadi  asilimia 29 kwa sasa.

Hiyo ni tofauti na  mimba za utotoni ambako kiwango chake kimezidi kuongezeka kutoka asilimia 23 kwa mwaka 2012 na kufikia asilimia 27 kwa sasa.

Alisema Serikali itaendelea kupambana kupinga utumikishwaji watoto nchini.

“Lengo ni kuhakikisha kiwango cha asilimia 29 kinapungua kwa kiasi kikubwa kwa vile  moja ya jitihada zinazofanywa na Serikali ni kupambana na utumikishwaji wa watoto kwa kuanzisha mpango wa elimu bure na kuhamasisha mahudhurio ya watoto shuleni  kutokomeza ajira za utotoni,”alisema Possi.

Alisema sekta zinazoongoza kwa kuajiri watoto ni misitu, kilimo na uvuvi ambayo ina kiwango cha asilimia 92.1 ya watoto wote wanaojihusisha na shughuli za uchumi.

Dk. Possi alisema mgawanyiko wa  jinsia wa watoto wanaojihusisha na ajira kwenye sekta ya kilimo umeonyesha kuwa wavulana ni asilimia 94.3 ya wavulana wote na wasichana ni asilimia 89.6 ya wasichana wote.

“Matokeo ya utafiti ya utumikishwaji watoto kwa mwaka 2014 yamebaini kati ya watoto milioni 15 wenye umri kati ya miaka mitano hadi 17, watoto milioni 4.2 sawa na asilimia 29 wanatumikishwa kwenye kazi mbalimbali za  uchumi.

“Hivyo mwenendo wa utumikishwaji watoto umepungua kutoka asilimia 31 ya mwaka 2006 hadi asilimia 29 ya sasa,”alisema Possi.

Alisema kadri umri wa watoto unavyoongozeka ndipo watoto wanapoongezewa majukumu ya shughuli mbalimbali hivyo kuwanyima fursa mbalimbali za  elimu.

Mkurugenzi wa NBS, Dk. Albina Chuwa alisema Tanzania ni moja ya nchi iliyoingia mikataba ya  taifa kwa ajili ya kulinda haki za watoto na kupinga ukatili dhidi yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles