22.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

SEKTA YA SANAA IENDELEE KUWA RAFIKI KWA WANAWAKE

NA CHRISTOPHER MSEKENA


TUKIWA bado kwenye wiki ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake, sekta ya sanaa imeendelea kuwa kiwanda kinachoajiri vijana wengi hususani wasanii wa kike.

Sanaa za muziki na filamu zimekuwa kimbilio kwa watu wote wenye vipaji vya uimbaji na kuigiza sinema. Wasanii hao wameendelea kujiajiri na kutengeneza fedha nyingi kwa kazi zao kuwa bidhaa inayonunuliwa na mashabiki.

Nafasi ya mwanamke kwenye kiwanda cha sanaa imeendelea kuwa kubwa kadiri siku zinavyokwenda tofauti na miaka kadhaa iliyopita. Kitambo hicho mwanamke alikuwa na nafasi finyu ya kuonyesha uwezo wake kisanaa.

Kuwa msanii ilikuwa ni kosa katika familia nyingi zenye watoto wa kike. Mwanamke kazi yake ilikuwa ni kufanya shughuli za nyumbani, kuolewa na kutunza familia pekee.

Msichana akijihusisha na muziki au filamu alionekana mhuni, amekosa maadili na wakati mwingine wazazi waliwatishia kuwapa laana kwani hawakuwa radhi kuona watoto wao wa kike wakijiingiza kwenye sanaa.

Hali hiyo ilifanya tasnia ya muziki na filamu na sanaa kwa ujumla wake kuwa na wasanii wa kike wachache. Asilimia kubwa ya wasanii waliofanikiwa kwenye sanaa hizo ni wanaume.

Miaka michache iliyopita mitazamo ya familia nyingi ilianza kubadilika. Wazazi wakaanza kuwapa ruhusa watoto wao kufanya muziki au filamu au sanaa nyingine wanazozipenda.

Kupitia mastaa wakubwa wa kike waliofanikiwa kwenye muziki wa kizazi kipya. Tukaanza kuona wasichana wengi wakiibuka na kuonyesha vipaji vyao licha ya kukutana na changamoto nyingi.

Changamoto kubwa iliyopigiwa kelele sana na wadau ni ile ya rushwa ya ngono iliyoua vipaji vingi vya watoto wa kike.

Wengi wameonyesha ukomavu wa kuvumilia changamoto hizo kwa kulinda heshima zao na leo hii tuna furaha kujivunia wasanii kama Vanessa Mdee ,Nandy, Ruby, Linah, Shilole na wengine wengi ambao hivi sasa wamesimama kama mfano kwa chipukizi wengine wa kike.

Wakati tunaendelea kufurahia ongezeko la wasanii nyota wa kike kwenye sekta ya sanaa, tunapaswa kuendelea kutafakari zaidi namna ya nyingine nzuri ya kuruhusu wasanii wa kike wanapata nafasi ya kuonyesha uwezo wao.

Maana idadi ya wasanii wa kiume imeendelea kubwa kutokana na ukweli kwamba wanaume hawapitii changamoto nyingi kama wanazopitia wasanii wa kike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,305FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles