23.4 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Sekta ya Ardhi yajivunia mafanikio lukuki mika 60 ya Uhuru

*Migogoro 149,081 yatatuliwa, wananchi wapata makazi bora

*Yakusanya bilioni 735.8 ndani ya miaka 10

*Ekari 885,144 zatolewa kwa wawekezaji

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara inajivunia mambo sita ikiwemo kutatua kiutawala jumla ya migogoro 149,081. 

Ameyataja mambo mengine ni  kupanga, kupima ardhi, kuwezesha wananchi kuwa na makazi bora, kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi,kuboresha mifumo na kutengeneza fursa za uwekezaji.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Novemba 21,2021 jijini Dodoma, wakati akieleza mafanikio ya Wizara hiyo ndani ya miaka 60,Waziri Lukuvi amesema katika miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara Wizara yake, imeweza kutatua migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri Lukuvi amesema baada ya uhuru, utatuzi wa migogoro ya ardhi ulikuwa unafanyika kupitia mabaraza ya kimila na mfumo wa mahakama za kawaida.

“Hata hivyo, utatuzi wa migogoro ya ardhi kupitia mfumo wa mahakama ulibainika kuwa na changamoto za mrundikano wa mashauri na matumizi ya mbinu nyingi za kisheria katika utatuzi wa migogoro,”amesema Lukuvi.

Amesema kutokana na changamoto hizo, Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 ilielekeza uanzishwe mfumo mahsusi wa utatuzi wa migogoro ya ardhi.

“Hivyo, Sheria ya Mahakama za Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi Na. 2 ya mwaka 2002 (Sura ya 216) ilitungwa na kubainisha mfumo maalum wa utatuzi wa migogoro ya ardhi unaojumuisha Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji, Mabaraza ya Kata, Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa,”amesem Lukuvia.

Waziri Lukuvi amesema tangu kutungwa kwa sheria hiyo mwaka 2002, jumla ya mashauri 214,588 yalifunguliwa na mashauri 187,618 yameamuliwa.

Aidha, amesema Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya yameanzishwa katika Wilaya zote 139 ambapo kati ya hayo, Mabaraza 60 yanatoa huduma. Dhamira ya Wizara ni kuhakikisha kuwa Mabaraza katika Wilaya zote nchini yanatoa huduma. 

Amefafafnua zaidi kuwa wizara imeendelea kushughulikia migogoro ya ardhi ambayo imekuwa kero kubwa nchini kadri inavyojitokeza kwa njia ya kiutawala.

Amesema  Migogoro hiyo ipo katika sura mbili ambazo ni migogoro ya mipaka ya kiutawala na migogoro inayotokana na mwingiliano wa matumizi ya ardhi.

Aidha, kupitia tathmini iliyofanyika imebainika kwamba vyanzo vya migogoro ni pamoja na ongezeko la watu, na mwingiliano wa matumizi ya ardhi kutokana na mahitaji mbalimbali ya watumiaji.

Wizara imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali ya kushughulikia utatuzi wa migogoro ya ardhi nchini.

Ameitaja mikakati hiyo ni pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu utatuzi wa migogoro kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa.

Pia, kuanzisha madawati ya malalamiko katika ofisi za ardhi za halmashauri nchini pamoja na programu ya ‘Funguka kwa Waziri.

Ameyataja mafanikio mengine ni: “Tumepanga; Tumepima; Tumemilikisha; tumewawezesha wananchi kuwa na makazi bora; Tumeboresha mifumo; Tumetengeneza fursa za uwekezaji; Tumeweka mfumo mzuri wa utatuzi wa migogoro na tumesogeza huduma za ardhi karibu kabisa na wananchi.  

Waziri Lukuvi amesema jumla ya maeneo 496 yametangazwa kuwa ya kupangwa nchini.

Amesema kutangazwa kwa maeneo hayo kumewezesha kupangwa, kuendelezwa na kusimamiwa kimji kwa kuzingatia Sheria ya Mipango miji Sura ya 355. iii)

Aidha, katika maeneo yalioendelezwa kiholela na ambayo yalikuwa ni mtaji mfu kwa wananchi tumerasimisha makazi 1,992,245 na kuwezesha wananchi hawa kuwa rasmi, usalama wa milki zao, na hadhi ya kukopesheka.  

Amesema kuipanga ardhi kumewezesha upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya kujenga uchumi shindani wa viwanda kwa maendeleo ya watu. 

“Katika kutimiza azma ya serikali ya kuwa na ardhi ya uwekezaji, ardhi yenye ukubwa wa ekari 885,144 zilitengwa na kumilikishwa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwa shughuli mbalimbali ikiwamo viwanda, kilimo, hoteli na biashara.

Pia ardhi yenye ukubwa wa ekari 224,439.4 zimetengwa kwa ajili ya uwekezaji kupitia Mipango Kabambe ya miji, mipango ya matumizi ya ardhi ya Wilaya na Vijiji,”amesema.

Vile vile,amesema wamesimika   mtandao wa alama za msingi za mfumo huo nchi nzima katika kila mkoa na kila wilaya kwa umbali wa kilomita 40.

“Hii imewezesha kila mahali kupimwa bila ya kuwa na shida za alama za kuanzia. Aidha, mfumo huu umepunguza gharama za upimaji na kuongeza kasi ya upimaji wa ardhi nchini,”amesema. 

Pia, wamenunua vifaa vya upimaji vya kisasa na kuvisambaza katika mikoa yote na baadhi ya halmashauri.

hizo kumewezesha wananchi kupata huduma za ardhi karibu na maeneo yao, kwa wakati na pia kupunguza gharama za kupata huduma hizo. Ili kuimarisha usimamizi wa sekta ya ardhi kwa ufanisi zaidi, mwaka 2018 Serikali iliwahamisha watumishi wa sekta ya ardhi waliokuwepo katika halmashauri mbalimbali kuwa chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kiutendaji maafisa hao wanafanya kazi kwa karibu za mamlaka za upangaji ambazo ni Halmashauri. 

Aidha,Waziri Lukuvi amesema umilikishaji wa ardhi kwa wananchi umewapa fursa wananchi kuchangia pato la Taifa.

MIAKA 10 MAKUSANYO BILIONI  735.8

Waziri huyo amesema Wizara inakusanya maduhuli ya sekta ya ardhi kutoka katika vyanzo mbalimbali kama vile, kodi ya pango la ardhi,ada za upimaji wa ardhi na Machapisho Mbalimbali,ada ya uthamini,ada za usajili wa hati na Nyaraka Mbalimbali.

Amesema Mwaka 1996/97 wakati Wizara ya Ardhi ilipopewa  mamlaka ya kukusanya maduhuli yatokanayo na sekta ya ardhi walikusanya  shilingi bilioni 1.4.                

“Kwa miaka 10 ya hivi karibuni (Juni, 2011 hadi Jalai, 2021) tumekusanya jumla ya shilingi bilioni 735.8,”amesema 

“Maduhuli yatokanayo na sekta ya ardhi yameongezeka kutoka shilingi bilioni 1.4 kwa mwaka wa fedha 1996/97 hadi kufikia shilingi bilioni 121 katika mwaka wa fedha 2020/21.

MALENGO

Amesema kwa mwaka huu (2021/2022) wana  malengo ya kukusanya bilioni 221 huku akidai matarajio ni kuhakikisha sekta hii inachangia zaidi katika pato la Taifa ikiwemo mapato ya kodi.

MWELEKEO   

Waziri lukuvi amesema Mwelekeo wa sekta hiyo  katika kipindi cha miaka ijayo ni kuwahakikishia wananchi na taasisi zote nchini usalama wa milki zao kwa kuwapatia hatimiliki za ardhi na huduma zingine muhimu za ardhi na hivyo, kudhibiti migogoro baina ya watumiaji ardhi.

“Azma hii itafikiwa kwa kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020-25 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa 2021/222025/26,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles