SEKTA BINAFSI ZATAKIWA KULINDA USAWA WA KIJINSIA

0
781

Na Veronica Romwald , Dar es salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga, amezitaka kampuni zote zilizopo katika sekta binafsi kuwekeza nguvu zaidi katika kulinda haki ya usawa wa kijinsia.

Nkinga ameyasema hayo leo Alhamisi Machi 8, jijini Dar es Salaam wakati akizindua kampeni ya kuhamasisha usawa wa kijinsia katika nyanja ya kiuchumi iliyoshirikisha Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Wanawake (UN-Women-Tanzania.

Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez amesema ikiwa dunia inahitaji kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) kila nchi inapaswa kumaliza tofauti za kijinsia zilizopo.

Naye, Mwakilishi wa UN Women (OIC), Hodan Addou alisema jitihada zinahitajika kufanyika sasa ili kukabili pengo la usawa wa kiuchumi lililopo duniani.

“Inakadiriwa itachukua zaidi ya miaka 217 kukabili pengo lililopo, lakini tusisubiri muda huo lazima tuanze sasa kuhimiza usawa,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here