24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Sekta binafsi zaombwa kuboresha mazingira

chatoNa MWANDISHI WETU

SEKTA binafsi nchini zimetakiwa kuunga mkono mikakati ya Serikali katika kuboresha mazingira ya kujifunzia shuleni.

Wito huo ulitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Shaaban Ntarambe, wakati wa kupokea vifaa vya maabara vyenye thamani ya Sh milioni 30 vilivyotolewa na Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Tigo katika shule ya Sekondari ya Chato ya wilayani humo.

Alisema ni jambo la kupongezwa lililofanywa na kampuni hiyo na kuongeza kuwa sekta nyingine binafsi nchini hazina budi kuiga mfano huo ili kuunga mkono jitihada hizo za Serikali.

“Naipongeza kampuni ya Tigo kwa ukarimu wake wa kusaidia shule hizi na pia napenda kutoa wito kwa watu binafsi, wafanyabiashara na wadau wengine kujitokeza na kujiunga na juhudi hizi zinazoendelea katika kuboresha elimu,” alisema Ntarambe.

Naye Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Edgar Mapande, akizungumza wakati wa sherehe ya makabidhiano hayo yaliyofanyika shuleni hapo, alisema kampuni hiyo itaendelea kuthibitisha namna ilivyojikita kuendeleza elimu nchini.

“Vifaa hivi vitatumika kikamilifu na wanafunzi ili kuwawezesha kuyafikia malengo yao ikiwamo pia kusaidia vifaa kwa ajili ya masomo ya sayansi ambayo wanafunzi wengi wamekuwa wakiyakimbia kutokana na changamoto ya vifaa vya kujifunzia,” alisema Mapande.

Akipokea vifaa hivyo, mkuu wa shule hiyo, Selema Bernardo, alisema vifaa hivyo vitawawezesha wanafunzi kuwa katika ngazi moja na wenzao wa shule nyingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles