27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Sekta binafsi nchini yashauriwa kutumia fursa zilizopo

Na Leonard Mang’oha, Mtanzania Digital

Sekta binafsi nchini imeshauriwa kutumia fursa zilizopo kwa kuwekeza katika uzajishaji umeme unaotokana na nishati jadidifu ili kuwezesha upatikanaji wa huduma hivyo kwa wananchi wanaoishi katika maeneo yasiyofikiwa na gridi ya taifa.

Ushauri huo umetolewa Jumamosi Machi 19, na Meneja Mkuu wa kampuni ya kuzalisha umeme ya Mwenga Hydro Limited, Deogratias Massawe, ya mkoani Iringa inayozailisha zaidi ya megawati sita kwa kutumia maji na upepo.

“Tunawakaribisha, kwa sababu ni sekta inayokuwa, lakini  kwa sababu sisi tumeitika kwenye nishati jadidifu niwahimize wawekeze katika nishati jadidifu kuliko kwenda vypp vingine ambavyo siyo ragiki wa mazingira,” amesema Massawe.

Hata hivyo Massawe ishauri Mamlaka ya udhibiti Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kuongeza uwazi katika utekelezaji wa kazi zake ikiwa ni pamoja na kanuni na sheria ili zieleweke kwa wadau wakuwamo wawekezaji.

Pia amelishauri Shirika la Umeme nchini (Tanesco)  kuendelee kuthamini na kutambua umuhimu wa miradi midogo midogo ya kuzalisha umeme inayotekelezwa na kampuni mwishoni mwa gridi ya Taifa kutokana na miradi hiyo kusaidia kuimarisha gridi na kupunguza upotevu wa umeme.

Aidha ameishauri Serikali kuangalia namna ya kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta ya umeme hususan nishati jadidifu kutokana na sekta hiyo kuwa na uwanja mpana wa kuboresha maisha ya wananchi na mazingira ya kibinadamu ya nchi.

“Kwa umeme huu ni rafiki wa mazingira, lakini pia mwisho wa gridi kuna wananchi wengi hawana umeme wanapata umeme kutoka kwenye hizi kampuni au taasisi za umeme mdogo. Unafuu wa kwanza wananchi wanapata huduma za umeme zilizo bora kwa mazingira wanayoishi kwa bei nafuu kuliko vyanzo vingine kama kuni na mkaa ambavyo  siyo rafiki kwa mazingira ya nchi yetu,” amesema Massawe.

Kwa upande wake mdau wa masuala ya mazingira, BenedictKyaruzi, amesema kuendelea kutumia nishati kama vile mafuta kuzalishia umeme na kuendelea magari kutaendelea kuchangia uchafuzi wa mazingira na kuharibu tabaka la juu la anga na kuongeza joto duniani.

“Kuchelewa kuondoka ni tatizo na ndiyo maana jitihada zinaendelea kufanyika, katika siku za karibuni nimeona baadhi ya magari yamefungwa mfumo wa umeme ili yatumie kiasi kidogo cha mafuta na umeme naamini utafika wakati tutakuwa na magari yanayotumia mafuta kidogo au yasiyotumia kabisa,” amesema Kyaruzi,” amesema Kyaruzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles